Pata taarifa kuu

Wanajihadi wateka mji wa Palma nchini Msumbiji

Baada ya mapigano ya siku tatu katika mji wa Palma kati ya wanajeshi na wanajihadi wa Kiislamu, wanaojiita Al Shabab, katika mkoa wa Cabo Delgabo ambao umeendelea kushuhudia mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2017 mji huo sasa umetekwa na magaidi hao.

La ville de Palma est située dans le nord-est du Mozambique et seulement à dix kilomètres du mégaprojet gazier piloté par le groupe français Total.
La ville de Palma est située dans le nord-est du Mozambique et seulement à dix kilomètres du mégaprojet gazier piloté par le groupe français Total. © capture d'écran Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi hao sasa wanadhibiti mji huo wenye wakaazi wa watu 75,000 wengi wao Waislamu.

Mashuhuda katika mjio huo wa Palma wanasema watu wamekuwa wakiuawa kwa kukatwa vichwa huku makaazi ya watu yakiteketezwa na mitambo ya mawasiliano ya simu ikiharibiwa.

Mwajiri wa mmoja aliyekuwa anasafiri kwenye mji wa Pemba amesema hajawasiliana na wafanyikazi wake tangu mapigano hayo, Jumatano iliyopita.

Wafanyikazi wa kigeni na watumishi wa serikali wapatao 200 waliolazimika kutafuta hifadhi katika hoteli moja, waliokolewa Ijumaa iliyopita katika hoteli hiyo iliyoshambuliwa.

Palma ndio mji pekee nchini Msumbiji ambao kwa sasa ndio unaodhibiti na wanajihadi, baada ya mji wa Bandari wa Mocímboa da Praia kuwa mikononi mwa wanajihadi mwezi Agosti mwaka 2020.

Kampuni ya Ufaransa, Total imetangaza kurejelea kazi zao katika mkoa huo wa Cabo Delgado ambao mashiriki ya kiraia yanasema watu 2600 wameuawa huku wengine 670,000 wakikimbia makwao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.