Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Zoé Kabila, mdogo wa rais wa zamani, atimuliwa mamlakani

Zoé Kabila, mdogo wa rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, amefukuzwa kwenye nafai ya gavana wa mokoa wa Tanganyika. Wengi mwa wabunge walipoga kura ya kutokuwa na imani naye. Lakini baadhi wamepinga hatua hiyo, akidai kwamba haikufuata sheria.

Zoé Kabila hapa ilikuwa mwezi Februari 2012 huko Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu)
Zoé Kabila hapa ilikuwa mwezi Februari 2012 huko Kinshasa. (Picha ya kumbukumbu) Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vyetu, Zoé Kabila Mwanzambala bado yuko Kinshasa, akizuiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani. Kukosekana kwake katika mkoa wa Tanganyika, hakuna mjumbe wa serikali yake aliyetaka kushiriki katika mkutano huo kujibu mashtaka yaliyomo katika hoja ya kutokuwa na imani naye.

Katika sehemu kulikofanyika mkutano huo, walikuepo wabunge 13 tu ambao walitoa hoja hiyo na ambao wanalaani usimamizi mbaya, ubadhirifu na ukosefu wa uongozi.

Hoja hii iliwasilishwa Jumanne kwa ajili ya mjadala uliyopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii. Wabunge wengine 12 wa Bunge la mkoa walisusia mkutano huo, wakibaini kwamba walikuwa wanajua matokeo. Mkakati uliowekwa kwa matumaini ya kubatilisha hatua ya kutimiliwa gavana Zoé Kabila na timu yake, amesema mmoja wa wajumbe wa tawi la kundi la AFDC-A wanaoendelea kumuunga mkono rais mpya wa Seneti Modeste Bahati Lukwebo, mwanachama wa Muungano mtakatifu wa taifa kutoka kamni ya Rais wa sasa Félix Thisekedi.

Kwa upande wa Mbunge Claudel Lubaya na mawaziri wa zamani Marie-Ange Mushobekwa na Geneviève Inagosi, wanasema sheria haijaheshimishwa. Kwa sasa wanasubiri uamuzi wa Mahakama ya  Katiba, ambayo inatarajia kutoa uamuzi kuhusiana na kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.