Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRICA YA KATI - USALAMA

UN – Yatuhumu wanajeshi wa Urusi nchini Jamhuri ya Africa ya Kati.

Watalaamu wa Umoja wa mataifa wametuhumu wanajeshi wa Urusi, wanaohudumu nchini Jamhuri ya Africa ya Kati, kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia na kutekeleza mauwaji ya kibaguzi, madai ambayo tayari Moscow imekanusha.

wanajeshi wa Urusi, nchini Jamhuri ya Africa ya kati
wanajeshi wa Urusi, nchini Jamhuri ya Africa ya kati REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Jopo la watalaamu linalofuatilia hali katika maeneo ya vita barani Africa, Katika ripoti yake ya kursa 40, imesema imekusanya ushahidi wa kutosha wa kuwahusisha wanajeshi wa Urusi kwa ushirikiano na wale wa Jumhuri ya Africa ya kati kuteleza vitendo vya kihalifu katika taifa hilo.

Ripoti hiyo pia imesema wanajeshi wa Urusi hawakutaka kuongozwa na wenzao wa CAR, wakati wakiendesha operesheni kali dhidi ya waasi, wanaohusishwa na rais wa zamani wa taifa hilo Francois Bozize.

Bozezi mwaka uliopita alijaribu kuzuia uchaguzi kufanyika nchini humo, mbali na madai ya kutaka kupindua serikali ya rais Faustin Archange Touadera.

Msemaji wa Mascow, Dmitry Peskov, amekanusha madai ya wanajeshi wa Urusi kuhusika na mauwaji ya raia na kuteketeza makaazi yao.

Jamhuri ya Africa ya Kati, ambayo ni taifa tajiri kwa madini limeshuhudia vurugu za kikabili na dini Tangu mwaka 2013, serikali ikikubaliana na kutia mkataba wa amani na waasi mwaka 2019, ila mkataba huo unaonekana kukosa kuetekelzwa kutoka na vitendo va vurugu kuendelea kutekelezwa, na makundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.