Pata taarifa kuu
WHO-AFRICA-COVID 19

WHO yaonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya Covid 19 barani Afrika

Shirika la afya duniani WHO linasema bara la Afrika limeshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya corona wiki hii, kufuatia kusambaa kwa virusi aina ya Delta, vilivyoanzia nchini India.

Mhudumu wa afya akitoa huduma kwa mgonjwa wa Covid 19 katika hospitali moja katika Kaunti ya Machakos nchini Kenya
Mhudumu wa afya akitoa huduma kwa mgonjwa wa Covid 19 katika hospitali moja katika Kaunti ya Machakos nchini Kenya AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo barani Afrika, Daktari  Matshidiso Moeti, amesema bara hilo linatarajia kushuhudia siku ngumu katika wiki zijazo, baada ya watu zaidi ya 250,000 kuambukizwa wiki hii pekee.

Kwa bara la Afrika, hali mbaya bado inatarajiwa kushudiwa kwa  sababu ya wimbi la tatu linaloshuhudiwa kwa sasa Changamoto ni kuwa tunatarajia kushuhudia ongezeko kubwa la maambukizi katika wiki kadhaa zijazo, na hali ya sasa inaonekana kuwa mbaya ikilinganishwa na kile kilichoshuhudiwa kwenye ukanda hapo awali.

Kutokana na hatua hii, WHO sasa inayataka mataifa ya Afrika kuwahimiza wananchi wake kuheshimu masharti ya kuzuia maambukizi ya corona na kuhakikisha kuwa chanjo zinapatikana.

Baadhi ya mataifa ambayo wiki hii yameshuhudia hali ngumu ya kulemewa na wagonjwa ni pamoja na Namibia na Tunisia.

 

Mpaka sasa ni chini ya asilimia mbili tu ya waafrika ndio waliopokea chanjo kamili ya kuzuia maambukizi ya virusi hivyo, wakati huu, watu wengi wakiendela kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.