Pata taarifa kuu
SAHEL-USALAMA

Mkuu wa majeshi ya Ufaransa ahitimisha ziara yake Sahel

Jenerali Thierry Burkhard ni Mkuu wa majeshi ya Ufaransa tangu mwezi Julai. Leo Jumapili anamaliza ziara ambayo ilimpeleka Chad, Niger, kisha Mali na suala lililojadiliwa ilikuwa kumalizika kwa Operesheni Barkhane.

Jenerali Thierry Burkhard ni Mkuu wa majeshi ya Ufaransa tangu mwezi Julai.
Jenerali Thierry Burkhard ni Mkuu wa majeshi ya Ufaransa tangu mwezi Julai. AFP - DANIEL COLE
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa Sahel ilichaguliwa kuwa kituo cha kwanza cha ziara yake, ni kwa sababu Mkuu wa majeshi ya Ufaransa alikuwa na ujumbe kwa nchi hizo. Huko N'Djamena alikutana na rais wa Baraza la Kijeshi la Mpito, Mahamat Idriss Déby, na katika nchi hizo tatu alizozuru - Chad, Niger na Mali alikutana na wakuu wa majeshi wa nchi hizo na hivyo kujadili haliya usalama katika ukanda wa Sahel.

Kwa nchi zote hizi, Jenerali Burkhard alitaka kuwahakikishia kuwa kumalizika kwa Operesheni Barkhane haihusiane kamwe na kumalizika kwa ushiriki wa Ufaransa katika ukanda wa Sahel. "Marekebisho hayo sio kuondoka, inapidi maneno haya yarejelewe ili kuondoa sintofahamu," amesema msemaji wa jeshi la Ufaransa Kanali Ianni, ambaye aliandamana na Jenerali Burkhard katika ziara yake huko Sahel.

Ikiwa kipaumbele cha Ufaransa kinabaki kuwa vita dhidi ya ugaidi, kumalizika kwa Operesheni Barkhane, na kutoka kwa zaidi ya wanajeshi 5,000 hadi 2,500-3,000, kunaashiria kuingia kwa mantiki ya "ushirikiano wa kiutendaji na usaidizi katika vita, "ambao utategemea hasa kikosi cha jeshi la Ulaya Takuba. Estonia, Jamhuri ya Czech na Italia tayari wamejikubalisha kuchangia katika kikosi hiki, Ureno, Denmark na Hungary hivi karibuni zitajiunga na kikosi cha Takuba.

Hata hivyo, kwa sasa inakadiriwa kuwa kikosi cha Takuba kina wanajeshi 700 tu, wakati Ufaransa inatarajia kuondoa wanajeshi zaidi ya 2000. "Hatuzungumzii juu ya kitu kimoja", amejibu msemaji wa majeshi ya Ufaransa, ambaye amebaini kwamba kundi la wanajeshi 50 wa kikosi cha Takuba litandamana na kikosi cha wanajeshi 150 wa Mali.

Hakuna maelezo juu ya kuondolewa kwa askari wa Ufaransa katika ukanda wa Sahel, "kwa sababu za usalama," lakini kukamilika kwake bado kunatarajiwa mwishoni mwa mwaka huu. Kwa upande wa kambi za jeshi huko Kidal, Tessalit na Timbuktu, kaskazini mwa Mali, "zitaendelea kufanyakazi", lakini zitachukuliwa na wanajeshi wa jeshi la Mali au kikosi cha Umoja wa Mataifa, MiNUSMA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.