Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Maswali yaibuka kuhusu kurejea kwa Yahya Jammeh nchini Gambia

Yahya Jammeh, rais aliyetawala Gambia kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 20 na ambaye kwa sasa yuko uhamishoni, anaweza kurudi nchini, hata kusiriki kwenye uwanja wa kisiasa kulingana na duru kutoka Gambia.

Ingawa waangalizi wanadai kwamba Bwana Barrow alisema hapo zamani kwamba Bwana Jammeh yuko huru kurudi nchini, lakini ni vigumu kwa kiongoizi huyo wa zamani kurejea nchini kwani anakabiliwa na mashitaka ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Ingawa waangalizi wanadai kwamba Bwana Barrow alisema hapo zamani kwamba Bwana Jammeh yuko huru kurudi nchini, lakini ni vigumu kwa kiongoizi huyo wa zamani kurejea nchini kwani anakabiliwa na mashitaka ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. GRTS - Gambia Radio and Television Services/AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia wengi wa Gambia walishtuka waliposikia kuwa kumefanyika muungano kati ya chama cha kiongozi wa zamani Yahya Jammeh na chama cha mrithi wake Adama Barrow.

Wakati rais wa sasa anatafuta muhula mwingine katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba, muungano huu unaleta hofu juu ya utayari wa kumshtaki kiongozi huyo wa zamani kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Katibu mkuu wa chama cha APRC cha Yahya Jammeh, Fabakary Tombong Jatta anasema chama chake kilifikia mkataba na Chama cha rais Adama Barrow (NPP) kumuunga mkono katika uchaguzi wa urais wa Desemba 4.

Je! Ni nini kinatokea na kwanini sasa?

Rais wa sasa Adama Barrow anawania muhula mwingine katika uchaguzi wa Desemba baada ya miaka mitano madarakani.

Bwana Barrow anaona kwamba chama chake, NPP, hakiwezi kushinda uchaguzi ujao peke yake kutokana na mdororo wa kiuchumi uliosababishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali, ukosefu wa ajira na visa vya raia kuitoroka nchi hiyo na kukimbilia Ulaya kutafuta maisha bora.

Ingawa waangalizi wanadai kwamba Bwana Barrow alisema hapo zamani kwamba Bwana Jammeh yuko huru kurudi nchini, lakini ni vigumu kwa kiongoizi huyo wa zamani kurejea nchini kwani anakabiliwa na mashitaka ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.