Pata taarifa kuu
ANGOLA

Angola: Rais wa zamani José Eduardo dos Santos arejea Luanda

Rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos amerejea nchini kimya kimya ili isije kuzua mtafaruko, kulingana na vyanzo rasmi kutoka serikali ya Angola.

José Eduardo dos Santos, rais wa zamani wa Angola.
José Eduardo dos Santos, rais wa zamani wa Angola. AMPE ROGÉRIO/LUSA
Matangazo ya kibiashara

Miaka miwili baada ya kuondoka kwenda Uhispania, rais wa zamani José Eduardo dos Santos yuko nchini Angola tangu Jumanne, Septemba 14, 2021, wakati watu kutoka familia yake, hasa binti yake Isabel dos Santos, anakabiliwa na mashitaka ya ufisadi mahakamani.

Kurejea kwa José Eduardo dos Santos kulitangazwa mara kadhaa, lakini hakuweza kutokea. José Eduardo dos Santos, alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa miaka 38. Rais wa zamani pia analindwa kikatiba. Hadhi yake kama mkuu wa zamani wa serikali inazuia mashtaka yoyote ya jinai hadi mwaka 2022.

Wakati mtoto wake, José Filomeno, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa ubadhirifu wa mali ya umma, na binti yake Isabel anashukiwa katika visa vingi vya ufisadi, je, rais wa zamani anakuja kujadili? Kurudi huku bila shaka kuliidhinishwa na rais wa sasa wa Angola na waziri wa zamani wa ulinzi wa dos Santos, Joao Lourenço. Ni yeye ambaye, baada ya kuchaguliwa kuwa rais na kiongozi wa chama cha MPLA, chama tawala, alianzisha mashtaka dhidi ya watu kutoka familia ya rais huyo wa zamani.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya siasa Olívio Kilumbo, licha ya kuishi uhamishoni kwa miaka miwili, kwa sababu za kiafya, José Eduardo dos Santos bado ana nguvu halisi ya ushawishi: "Anapendwa na Waangola wengi, kwa sababu ndiye rais wa zamani ambaye badoyupo hai. Kwa hivyo sauti yake ni muhimu nchini Angola, kwa sababu anaweza kufaulu kwa kutekeleza jukumu la ushawishi mzuri au kuzidisha mivutano, "amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.