Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Nasser al-Tergui, kiongozi wa GSIM Gourma, auawa na kikosi cha Barkhane

Habari hiyo imetolewa Alhamisi hii, Oktoba 21, 2021 na makao makuu ya jeshi la Ufaransa. Nasser al-Tergui alikuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika kundi la GSIM linalodai kutetea Uislamu na Waislamu, kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda.

Helikopta za kikosi cha Barkhane nchini Mali.
Helikopta za kikosi cha Barkhane nchini Mali. MICHELE CATTANI AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Kuuawa kwake, Jumamosi hii, Oktoba 16, 2021, kunakuja tu wakati serikali ya Bamako imetangaza kwamba imeipa mamlaka taasisi kuu ya dini ya Kiislamu ya Mali kujadiliana na kundi la kigaidi.

Nasser al-Tergui alikuwa afisa mkuu wa kundi la waasi la GSIM, namba mbili wa kundi la Katiba Gourma Serma na mkuu wa tawi la kundi hilo katika eneo la Gourma.

Ijumaa, Oktoba 15, Barkhane iliona gari lililobeba watu 5 kaskazini magharibi mwa Gossi. Vyanzo mbalimbali vya ujasusi viliwezesha ili atambuliwe kuwa miongoni mwa watu hao. Gari hilo lilielekea baadaye katika mji wa Hombori kusini mwa nchi. Jumamosi, Oktoba 16, mashambulio mawili ya anga yalizinduliwa na kundi la makomando lilisafirishwa kwa helikopta katika eneo hilo kwa minajili ya kutambua walioangamia katika mashambulizi hayo.

Wakati Bamako inaanzisha mazungumzo nawanajihadi wa kundi la GSIM, kuuawa kwa Nasser al-Tergui kunasikika kama jibu kutoka Paris, ambayo inaona kuwa ufunguzi wa mazungumzo kama hayo ni msatari nyekundu. Alhamisi hii, mawaziri wa ulinzi wa NATO wanakutana Brussels: Ufaransa inaonyesha kwamba ndani ya muungano huo, nchi za Ulaya ambazo zimejiunga na kikosi cha Takouba ziko katika mstari huo na kwamba Marekani katika miezi ya hivi karibuni imeimarisha msaada wake kwa kikosi cha Barkhane. Pia ni kupitia msaada wa ujasusi wa Marekani, aliangamizwa Nasser al-Tergui, imebainisha Wizara ya Jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.