Pata taarifa kuu
NIGER-USHIRIKIANO

Niger: Rais Mohamed Bazoum aunga mkono jeshi la Ufaransa

Msafara wa magari ya kijeshi ya Ufaransa ambao ulikuwa umekwama kwa zaidi ya wiki moja nchini Burkina Faso uliwasili Niger siku ya Ijumaa (tarehe 26 Novemba). Rais Mohamed Bazoum amechukua fursa hiyo kupongeza kujitolea kwa wanajeshi wa Ufaransa katika ukanda wa Sahel wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Rais wa Niger, Mohamed Bazoum, anaunga mkono jeshi la Ufaransa lililotumwa Sahel.
Rais wa Niger, Mohamed Bazoum, anaunga mkono jeshi la Ufaransa lililotumwa Sahel. Michele Cattani AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati akikaribisha ushirikiano mzuri wa kijeshi kati ya Niger na washirika wake watano katika vita dhidi ya ugaidi, rais Mohamed Bazoum amekaribisha hasa kujitolea kwa Ufaransa katika ukanda wa Sahel: "Kati ya nchi zote zinazojitolea kwa upande wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi, Ufaransa ni nchi kima mtu anona juhudi zake. Wanajeshi 53 wa Ufaransa walifariki nchini Mali, amekumbusha rais huyo. Nimesikia watu wakisema kuwa Wafaransa wapo katika kanda huuu lakini matatizo hayajatatuliwa na kubaii kwamba wao ndio wanahusika na matatizo hayo. Na ikiwa Wafaransa wataondoka, una uhakika kwamba majeshi haya, ambayo yana wajibu wao leo, yataweza kukabiliana na hali hii? Hapana ! Nina hakika kwamba siku Wafaransa watakapo fungaha virago vyao huko Gao, hali itakuwa nzito kabisa! Wakazi wa Gao wanajua hilo”.

Kampeni dhidi ya Ufaransa inafanywa, kulingana na Rais Bazoum

Ni wazi na kwa uwajibikaji wote kwamba rais Mohamed Bazoum anapinga kampeni za dhuluma dhidi ya Ufaransa na jeshi lake katika ukanda wa Sahel: "Ninasikitika kabisa kwa kampeni inayofanywa dhidi yao. Nataka Wafaransa wawe na faraja, kwa sababu wana historia ya kipekee katika eneo hili la Sahel ..."

"Hadi sasa, bataliani kumi na mbili vya vikosi maalum vya Niger vimepewa mafunzo na Canada, Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.