Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Jeshi la Ufaransa: Wanajihadi sitini wauawa Burkina Faso

Kati ya Januari 16 na 23, makundi mbalimbali ya magaidi vilionekana, kutambuliwa na kuangamizwa na vikosi vya Burkina Faso na vitengo vya jeshi la Ufaransa, Barkhane, vinavyoendesha shughulizi hizo katika ukanda huo.

Vikosi vya operesheni Barkhane vikiendelea na vita dhidi ya makundi ya magaidi katika ukanda wa Sahel..
Vikosi vya operesheni Barkhane vikiendelea na vita dhidi ya makundi ya magaidi katika ukanda wa Sahel.. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi 60 waliuawa kaskazini mwa Burkina Faso wakati wa operesheni iliyoongozwa na vikosi vya Burkina Faso, wakisaidiwa na vitengo vya Ufaransa vya Operesheni Barkhane, makao makuu ya jeshi la Ufaransa yametangaza Jumapili.

 

"Vikosi vya Barkhane na vikosi vya jeshi vya Burkina Faso vilifanya operesheni ya pamoja kaskazini mwa Burkina Faso kuanzia Januari 15 hadi 23. Magaidi sitini waliangamizwa. Mapambano dhidi ya makundi yenye silaha yanaendelea,” makao makuu ya jeshi (EMA) yameadika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Matokeo ya operesheni hii yanaonyesha ahadi na dhamira ya Barkhane na washirika wake wote kuendeleza mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi yenye silaha", imebaini taaifa kutoka makao makuu ya jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.