Pata taarifa kuu

Jeshi la Ufaransa latangaza kuwaua wanajihadi 40 nchini Burkina Faso

Wanajeshi wa Ufaransa katika operesheni dhidi ya wanajihadi Barkhane wamewaangamiza wanajihadi 40 nchini Burkina Faso waliohusika katika mashambulizi ya hivi majuzi kaskazini mwa nchi jirani ya Benin na kusababisha vifo vya watu 9 akiwemo mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa.

Kikosi cha Barkhane, ambacho " kimepewa tahadhari na washirika wake wa Benin na Burkina Faso", "kilitoa uwezo wa kijasusi wa anga kutafuta kundi hili lenye silaha" lililohusika na mashambulizi kabla ya kufanya mashambulizi ya anga siku ya Alhamisi ambapo wanajihadi hao waliuawa, inaeleza taarifa.
Kikosi cha Barkhane, ambacho " kimepewa tahadhari na washirika wake wa Benin na Burkina Faso", "kilitoa uwezo wa kijasusi wa anga kutafuta kundi hili lenye silaha" lililohusika na mashambulizi kabla ya kufanya mashambulizi ya anga siku ya Alhamisi ambapo wanajihadi hao waliuawa, inaeleza taarifa. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mashambulizi matatu ya mabomu yaliyotengenezwa kienyeji, Jumanne na Alhamisi, ambayo yalisababisha vifo vya watu 9 akiwemo raiammoja wa Ufaransa na 12 kujeruhiwa kaskazini mwa Benin, jeshi la Ufaransa limewaangamiza wanajihadi 40 waliohusika katika mashambulizi hayo nchini Burkina Faso, makao makuu ya jeshi yametangaza leo Jumamosi katika taarifa.

Kikosi cha Barkhane, ambacho " kimepewa tahadhari na washirika wake wa Benin na Burkina Faso", "kilitoa uwezo wa kijasusi wa anga kutafuta kundi hili lenye silaha" lililohusika na mashambulizi kabla ya kufanya mashambulizi ya anga siku ya Alhamisi ambapo wanajihadi hao waliuawa, inaeleza taarifa.

"Asubuhi ya Februari 10, baada ya kupata na kutambua safu ya kwanza ya magaidi waliokuwa wakisafiri kwa pikipiki, kwa makubaliano na kwa uratibu wa kudumu na mamlaka ya Burkina Faso, shambulio la kwanza la anga lilifanywa na ndege isio na rubani ya Reaper wakati safu hiyo ilikuwa tayari imeingia nchini Burkina Faso ", na "magaidi kadhaa wameangamizwa", kulingana na makao makuu ya jeshi.

Benin hadi hivi majuzi ililikuwa ikichukuliwa kuwa kisiwa cha utulivu katika Afrika Magharibi, eneo ambalo makundi mengi ya kijihadi yanavyohusishwa na Al-Qaeda na kundi la Islamic State (IS) yanaendesha harakati zao. Lakini mfululizo wa hivi majuzi wa mashambulizi ya anga kwenye mpaka katika nchi zilizo kusini mwa Sahel umethibitisha hofu kwamba makundi ya kijihadi yanayofanya kazi nchini Mali, Niger na Burkina Faso yanajaribu kusonga mbele kuelekea pwani.

Ufaransa, ambayo imekuwa ikipigana na makundi ya wanajihadi katika Sahel kwa miaka tisa, inaweza kutangaza vyema kuondoka kwa wanajeshi wake kutoka Mali katika siku zijazo, kwani utawala wa kijeshi huko Bamako unaonyesha kuongezeka kwa uhasama dhidi ya uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa.

Paris hata hivyo inabaki na nia thabiti ya kuendelea kupigana dhidi ya kuenea kwa makundi ya wanajihadi katika eneo hilo. Makao makuu ya jeshi la Ufaransa yanataka kuimarisha shughuli zake za ushirikiano huko na kutoa uwezo muhimu kwa makao makuu ya majeshi ya nchi za eneo hilo, kulingana na vyanzo vya kuaminika.

Kipaumbele cha Ufaransa kinasalia "kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi" pamoja na nchi za Kiafrika, Mkuu wa Majeshi ya Ufaransa, Jenerali Thierry Burkhard, alisisitiza Jumanne wakati wa ziara yake nchini Côte d'Ivoire.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.