Pata taarifa kuu
Cameroon - Siasa

Cameroon yaadimisha miaka 50 ya muungano

Raia wa Cameroon, leo wanaadimisha miaka 50 tangu kuja pamoja kwa upande wa Cameroon ya Magharibi na ile ya Mashariki, na baada ye kuunda taifa moja la Cameroon mwaka 1972.

Rais wa Cameroon Paul Biya (picha kumbukumbu)
Rais wa Cameroon Paul Biya (picha kumbukumbu) Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo taifa hilo limekuwa likishuhudia machafuko ya mara kwa mara kutoka kwa waasi wa upande wa Kaskazini magharibi eneo ambalo raia huzungumza kingreza, kujitenga na wanajeshi wa serikali.

Miaka ya awali siku hii ingeadimisha kwa wanajeshi kuandaa gwaride katika miji mbalimbali lakini hali imebadilika kutokana na eneo la Kaskazini magharibi, kutaka kujitenga.

Hata hivyo raia wengi wa Kaskazini magharibi hasa mji wa Bamenda, ambao umekuwa ukishuhudia machafuko mara kwa mara, wanashikiza serikali kushiriki mazungumzo na makundi yanayotaka kujitenga ili kumaliza mgogoro ambao umekuwepo kwa muda sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.