Misri - Mazingira
Misri : Yazindua mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Serikali ya Misri imezindua rasmi mpango wake wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, mpango huo ukitarajiwa kutumiwa hadi mwaka 2050.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Waziri mkuu wa taifa hilo Mustafa Madbouly, amesema Misri ni baadhi ya mataifa ambayo yameathirika pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi akihusisha hali hiyo na hatari ya usalama kwa taifa,kwani mabadaliko yatachangia umaskini na changamoto nyinginezo.
Haya yanajiri wakati huu taifa hilo likijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 27 wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mwezi novemba.