Pata taarifa kuu
Misri - Usalama

Misri : Wanawake wawili wafariki baada ya kushambuliwa na Papa

Mamlaka nchini Misri, zimesema wanawake wawili wameuawa baada ya kushumbuliwa na samaki aina ya Papa, wakati wakiogelea katika bahari ya shamu.

Samaki aina ya papa
Samaki aina ya papa Niranjan, sous Creative Commons Attribution
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mazingira nchini humo imesema vifo hivyo vilitokea umbali wa mitaa 600, raia wa Austria akifariki ijumaa kutokana na majiraha aliyopata baada ya kushambuliwa na papa.

Katika kisa kingine tofauti mwanamke mwenye umri wa miaka 40, raia wa Romania pia amefariki baada kushambuliwa na samaki aina ya papa.

Visa hiki vimeripotiwa katika eneo la Hurghada, eneo ambalo ni kivutio kikubwa cha watali nchini Misri, mamlaka zikilazimika kufunga baadhi ya maeneo kutokana visa hivyo viwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.