Pata taarifa kuu
ANGOLA- SIASA.

Mzozo waibuka juu ya mazishi ya José Eduardo dos Santos.

Mzozo umeibuka kuhusu mazishi ya rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos, aliyefariki siku ya Ijuma wakati akipokea matibabu katika hosipitali moja nchini Hisapania.

José Eduardo dos Santos, rais wa zmani wa Angola.
José Eduardo dos Santos, rais wa zmani wa Angola. LUSA - TIAGO PETINGA
Matangazo ya kibiashara

Mvutano huo umeibuka baada ya agizo la rais wa sasa João Lourenço la kutaka kuundwa kwa tume itayoshugulikia mipango ya mazishi ya mtangulizi wake jijini Luanda.

Agizo hilo la rais Lourenco limekataliwa na upande wa familia ya hayati Dos Santos, ikiongozwa na wanawe wa kiume kwa misingi kuwa Jose Eduardo alitaka azikwe mjini Barcelona bila ya kutoa sababu za kutaka kufanywa hivyo wakitaka ombi la baba yao kuheshimwa.

Welwitchia dos Santos, mwanawe wa kiume, naye pia amepinga mipangilio hiyo ya mazishi ya kitaifa kutokana na mvutano kati yao na serikali ya Angola.

Siku ya Ijuma rais João alisema kuwa serikali ya Angola itapanga mazishi ya matangulizi wake na kuwaalika watu wote wakiwemo watu wa karibu wa hayati Dos Santos walioishi katika nchini za kigeni.

Welwitchia pamoja na dada yake Isabel, anayekabiliwa na kesi za ufisadi katika mataifa tofauti, wamekuwa wakiishi nje ya Angola kwa madai ya kuhofia usalama wao pamoja na kusalitiwa kisiasa.

Matukio haya yanajiri wakati huu mamlaka katika mahakama za nchini Hisapania zikikubali wito wa mwanawe wa kike wa rais huyo wa zamani wa Angola la kutaka mabaki ya babake kufanyiwa uchunguzi wa maiti.

Baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 37, dos santos aliondoka uongozini mwaka wa 2017 na kumkabidhi madaraka rais wa sasa João Lourenco,rafiki wake wa muda mrefu . Mambo hayakuenda kama alivyotarajia santos baada ya mrithi wake kuaanza kumchunguza kwa madai ya kuhusika na ufisadi.

Dos santos, aliondoka nchini Angola Aprili 16 ,2019 kuelekea nchini Hisapania kutafuta matibabu ,ambapo aliishi kwa muda mrefu .

Rais huyo wa zamani wa Angola, alizaliwa Agosti 28, 1942 jijini Luanda katika manispa ya Sambizanga, japokuwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani pamoja na mashirika ya kiraia wakisema kuwa alizaliwa katika eneo la Sao Tome and Principe.

Hayati Dos Santos, aliweka historia baada ya kuingia madarakani akiwa na umri wa miaka 37. Aliondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi cha maika 37.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.