Pata taarifa kuu
ANGOLA- TANZIA

Uchunguzi umebaini kuwa Dos Santos hakuuawa- Mwanasheria Mkuu wa Angola

Mwanasheria Mkuu wa Angola Helder Pitta Gros amesema kuwa  uchunguzi wa maiti uliofanywa kwa mwili wa  aliyekuwa rais wa Angola José Eduardo dos Santos umebaini kuwa kiongozi huyo  hakuwekewa sumu kama ilivyokuwa imedaiwa awali .

Picha ya aliyekuwa rais wa Angola, José Eduardo dos Santos.
Picha ya aliyekuwa rais wa Angola, José Eduardo dos Santos. LUSA - AMPE ROGÉRIO
Matangazo ya kibiashara

Ijumaa iliyopita, Mahakama jijini Barcelona iliagiza kufanyika kwa uchunguzi kwenye mwili wa rais huyo wa zamani aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, baada ya kulazwa hospitalini Juni 23 baaada ya kupata mshtuko wa moyo.

Tchize dos Santos mwanawe wa kike wa rais huyo amabye aliongoza Angola kwa miaka 40 alikuwa ametoa ombi kwa mahakama nchini kutoa kibali cha kutaka mwili wa babake ufanyiwe ukaguzi wa maiti akidai kuwa huenda kulikuwa na njama fiche katika kifo chake.  

Mawakili wa familia hiyo wameshutumu hatua ya serikali ya Angola ya kutaka kurudisha mwili wa rais huyo wa zamani nyumbani kwa ajili ya mazishi ya kiserikali, familia ikitaja kitendo hicho kuwa kinyume na alivyotaka jamaa wao.

Mawakili wa familia  ya Dos Santos kwa niaba ya familia walikuwa wamehoji  ni kwanini mke wake, alitengwa na mgonjwa kwa muda lakini pia kumekuwa na madai ya kiongozi huyo kutoangaliwa vema alipokuwa hospitalini.

Wapinzani wa rais huyo wa zamani wamekuwa wakimkumbuka kama kiongozi aliyetmia utajiri wa mafuta nchini mwake kujitajirisha yeye na familia yake kwa kipindi chote alichokuwa madarakani.

Baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 37, dos santos aliondoka uongozini mwaka wa 2017 na kumkabidhi madaraka rais wa sasa João Lourenco,rafiki wake wa muda mrefu . Mambo hayakuenda kama alivyotarajia santos baada ya mrithi wake kuaanza kumchunguza kwa madai ya kuhusika na ufisadi.

Dos santos, aliondoka nchini Angola Aprili 16 ,2019 kuelekea nchini Hisapania kutafuta matibabu ,ambapo aliishi kwa muda mrefu .

Rais huyo wa zamani wa Angola, alizaliwa Agosti 28, 1942 jijini Luanda katika manispa ya Sambizanga, japokuwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani pamoja na mashirika ya kiraia wakisema kuwa alizaliwa katika eneo la Sao Tome and Principe.

Hayati Dos Santos, aliweka historia baada ya kuingia madarakani akiwa na umri wa miaka 37. Aliondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi cha maika 37.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.