Pata taarifa kuu
CAR- USALAMA

CAR: Kiongozi wa waasi Nourredine Adam anatakiwa na mahakama ya ICC

Mahakama ya kimataifa inayoshugulikia makosa ya uhalifu wa jinai (ICC) inasema kuwa imetoa amri ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati kutokana na vitendo vya kihalifu vilivyotekelezwa dhidi ya raia wakati wa machafuko ya mwaka wa 2013.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ICC, Karim Khan
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ICC, Karim Khan AFP - DANIEL MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Nourredine Adam, anatakiwa kwa makosa anayotuhumiwa kuyatekeleza wakati akiwa waziri wa usalama wakati huo.

Anatakiwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya kuwatesa raia, kuwafunga jela, kuwatowesha watu ikiwemo vitendo vya kikatili vilivyotendwa raia waliokuwa wanazuiliwa katika vituo vilivyokuwa vinamilikiwa na utawala wa wakati huo.

Jamuhuri ya Afrika ya kati ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya mapinduzi ya mwaka wa 2013 na licha ya mapigano kupungua, makundi ya waasi yangali yanatekeleza mashambulio nchini humo.

Adam kwa sasa ni kiongozi wa kundi la waasi la Popular Front for the Rebirth of the Central African Republic (FPRC), kundi la wapiganaji ambalo ndilo kubwa nchini CAR.

Kundi lake ni mojawapo ya makundi ya wapiganaji mawili nchini humo yaliokataa wito wa rais Faustin-Archange Touadera mwaka jana wa kusitisha mapigano.

Utawala wa kiraia uliokuwa unaongozwa na rais Francois Bozize,ulipinduliwa mwaka wa 2013 kabala yake kurejea tena madarakani mwongo moja baadae.

Mapigano yalizuka kati ya muungano wa makundi yenye silaha yalioongoza mapinduzi ya rais Bozize, na makundi ya waasi yaliokuwa yanamuunga mkono Bozize.

Wababe wengine wawili wa kivita nchini humo Patrice-Edouard Ngaissona na Alfred Yekatom, ambao waliongoza kundi la wapiganaji wa Balaka wanachunguzwa na ICC kwa kuhusika na makosa ya uhalifu wa kibindamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.