Pata taarifa kuu

Mali yaishutumu Ufaransa kwa kuwapa silaha magaidi na kuilalamikia Umoja wa Mataifa

Mali imejikuta tena katikae malumbano dhidi ya Ufaransa wakati huu, na kuwasilisha malalamiko yake mbele ya Umoja wa Mataifa. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, hapa akiwa Moscow mnamo Novemba 11, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, hapa akiwa Moscow mnamo Novemba 11, 2021. © Yuri Kochetkov / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati Ufaransa ikikamilisha zoezi la kuondoa kikosi cha Barkhane mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akilitaka kukemea ukiukaji wa anga ya Mali. Abdoulaye Diop pia analishutumu jeshi la Ufaransa kwa kuunga mkono wanajihadi. Taarifa hizo zilifichuliwa na wenzetu kutoka Jeune Afrique, lakini RFI pia iliweza kupata barua hii.

Shutuma za Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ni kubwa: Ufaransa imetoa silaha, risasi na taarifa za kijasusi kwa magaidi wa kijihadi wanaoendelea kuihujumu nchi ya Mali. Barua iliyoandikwa na Abdoulaye Diop ni ya tarehe 15 Agosti, waziri anaanza kwa kuorodhesha mfululizo wa kesi zilizowasilishwa kama "ukiukwaji wa mara kwa mara wa anga ya Mali na vikosi vya Ufaransa": "ndege sizokuwa na rubani, helikopta au ndege za kivita ziliruka juu ya anga ya Mali kutoka mji mkuu wa Mali, "bila idhini. ”

Takriban kesi hamsini zimeripotiwa kurekodiwa tangu kuanza kwa mwaka huu. Abdoulaye Diop anashutumu "shughuli za upelelezi" na, hasa, "vifurushi vilivyodondoshwa" na jeshi la Ufaransa, kama huko Labezanga mnamo Agosti 8.

Kwa mujibu wa Waziri Diop, Mali ingekuwa ina"ushahidi" unaothibitisha kwamba uvamizi huu usio halali katika anga ya Mali "umetumia Ufaransa kukusanya taarifa kwa manufaa ya makundi ya kigaidi" "na kuwaachia silaha na risasi. »

Wiki moja iliyopita, baada ya shambulio dhidi ya kambi ya Tessit ambayo iligharimu maisha ya wanajeshi 42 wa Mali, jeshi la Mali lilidai kuwa lilirekodi "operesheni za siri na zisizo na uratibu" na kuthibitisha kwamba magaidi - wa Kundi la Islamic State lilinufaika na "msaada mkuu kutoka nje. »

Ufaransa haijasema chochote kuhusiana na madai haya ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.