Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

G5 Sahel yatafuta "mkakati mpya" baada ya Mali kujiondoa

Mawaziri wa ulinzi na wakuu wa majeshi wa nchi za G5 Sahel walifanya mkutano usiokuwa wa kawaida mjini Niamey siku ya Alhamisi kutafakari juu ya "mkakati mpya" wa kikosi hiki cha kupambana na wanajihadi baada ya Mali kujiondoa mwezi Mei, shirika la habari la AFP limebaini Ijumaa wiki hii.

Wanajeshi wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel, katika eneo la In Tillit, Mali, wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema Novemba 2017.
Wanajeshi wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel, katika eneo la In Tillit, Mali, wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema Novemba 2017. RFI / Anthony Fouchard
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa siku moja ulilenga "kubadilishana kuhusu usanidi mpya" wa Jeshi la Pamoja baada ya "Mali kujiondoa" na "kuondoka kwa kikosi cha Barkhane" katika nchi hii, kulingana na taarifa ya mwisho. "Hali hii inatuhitaji kupitisha mikakati mipya ya kupambana vilivyo na makundi ya kigaidi yenye silaha katika anga ya pamoja", taarifa hiyo imeongeza.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu mkakati huu mpya. G5 Sahel ni kikosi cha pamoja cha kijeshi ambacho hadi mwezi wa Mei kilileta pamoja Niger, Burkina Faso, Mauritania, Chad na Mali.

Kwa kiasi kikubwa kikosi hiki kinachofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, kiliwakilishwa machoni pa washirika wa kimataifa katika Sahel njia ya kutoka katika eneo lililokumbwa na ghasia za wanajihadi. Lakini katika kipindi cha miaka mitano, operesheni za pamoja zimesalia chache kwa idadi na hali ya usalama katika ukanda wa Sahel imeendelea kuzorota.

Licha ya "juhudi" za Mataifa kwa "msaada" wa washirika, "hali ya usalama bado inatia wasiwasi, hasa katika eneo la 'mipaka mitatu'", kwenye mipaka ya Burkina, Mali na Niger, taarifa  hiyo imesisitiza.

"Mfumo wa sasa (...) hauwezi tena kukidhi matatizo yetu ya kiutendaji", alisema katika ufunguzi wa mkutano huo, Jenerali Gninguengar Mandjita, Mkuuwa Majeshi ya Chad, nchi ambayo inashikilia uwenyekiti wa G5 Sahel.

Alkassoum Indatou, Waziri wa Ulinzi wa Niger, anabaini kwamba "zaidi ya matatizo ya kifedha", G5 Sahel sasa inakabiliwa na "tatizo la mshikamano na umoja wa utekelezaji (...) uliodhoofishwa tangu kujiondoa kwa Mali".

Katikati ya mwezi wa Mei, mamlaka ya mpito nchini Mali, iliyozuiwa kushika kiti cha urais, iliamua kujiondoa kutoka kwa G5 Sahel na kikosi chake cha pamoja, ikitaja "kupoteza uhuru" na "utumiaji wa vyombo" ndani ya jumuiya. Mwezi Julai, rais wa Chad Mahamat Idriss Déby na mwenzake Mohamed Bazoum wa Niger walisisitiza kutaka kuweka hai G5, licha ya kuondoka kwa Mali.

Jeshi lililo madarakani tangu mwaka 2020 nchini Mali hivi karibuni liliishawishi Ufaransa kuondoka, ambayo ilituma maelfu ya wanajeshi wake nchini humo kwa miaka mingi kupitia operesheni yake ya Barkhane, ambao baadhi yao wanapiga kambi katika nchi jirani ya Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.