Pata taarifa kuu

Teodoro Obiang Nguema kuwania kiti cha urais kwa muhula wa 6 nchini Equatorial Guinea

Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, 80, ambaye ameitawala Equatorial Guinea kwa mkono wa chuma kwa miaka 43 na ambaye alikuwa hajawa na uhakika wa kugombea, hatimaye atawania muhula mpya katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba, makamu wa rais amesema Ijumaa kwenye ujumbe wa twitter.

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema anayetawala Equatorial Guinea tangu 1979, anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa madarakani kwa muda mrefu kwa wakuu wa nchi ambao bado wako hai, ukiondoa utawala wa kifalme.
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema anayetawala Equatorial Guinea tangu 1979, anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa madarakani kwa muda mrefu kwa wakuu wa nchi ambao bado wako hai, ukiondoa utawala wa kifalme. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Kwa sababu ya haiba yake, uongozi wake na uzoefu wake wa kisiasa (...)", chama tawala "kwa kauli moja kimemchagua ndugu mpambanaji Teodoro Obiang Nguema Mbasogo kuwa mgombea atakayewakilisha chama katika uchaguzi wa urais" mnamo Novemba 20, ameandika makamu wa rais, Teodoro Nguema Obiang Mangue, anayejulikana kwa jina la utani Teodorin, mtoto wa rais aliye madarakani.

Bw. Obiang, anayetawala Equatorial Guinea tangu 1979, anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa madarakani kwa muda mrefu kwa wakuu wa nchi ambao bado wako hai, ukiondoa utawala wa kifalme. Suala pekee katika uchaguzi huo lilikuwa katika uteuzi wa mgombea wa chama cha Democratic Party of Equatorial Guinea (PDGE), ambacho kinakalia viti 99 kati ya 100 vya bunge linalomaliza muda wake na viti vyote 70 vya Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.