Pata taarifa kuu

Ethiopia: serikali ya Ethiopia kushiriki kwenye mazungumzo na TPLF

Serikali ya Ethiopia imekubali ombi la Umoja wa Afrika, kushiriki kwenye mazungumzo ya amani na waasi wa Tigray, kujaribu kumaliza mapigano ambayp yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili.

Mpatanishi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia,Olesegun Obasanjo
Mpatanishi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia,Olesegun Obasanjo © REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

 

Redwan Hussein, mshauri wa masuala ya usalama kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa Twitter, amethibitisha serikali kukubali ombi hilo akisema inaendana na msimamo wa serikali wa kutaka mzozo huo kutatuliwa kwa amani.

Aidha, serikali ya Ethiopia imesema tayari Umoja wa Afrika umeandaa tarehe na eneo ambalo mazungumzo hayo yatafanyika lakini, taarifa za kina hazijawekwa wazi.

Msemaji wa Umoja wa Afrika Ebba Kalondo, naye hajaeleza kwa undani kuhusu ni wapi na lini mazungumzo hayo yatafanyika, akisema tu kuwa mchakato unaendelea.

Ripoti za kidiplomasia zinasema, mazungumzo hayo yataongozwa na mjumbe wa Umoja wa Afrika kwenye ukanda wa pembe ya Afrika, rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanja na aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, waasi wa Tigray hawajazungumzia kuhusu kauli ya serikali ya Ethiopia, mwezi mmoja baada ya mapigan kuzuka tena katika jimbo la Tigray, ambalo limeshuhudia maelfu ya watu wakipoteza maisha na mamilioni kuyakimbia makwao

Carol Korir amezungumza na Rashid Abdi, mchambuzi wa usalama kutoka kampuni ya  Sahan  Research , akiwa jijini Nairobi.

.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.