Pata taarifa kuu

Mgawanyiko wajitokeza kati ya kambi ya Moise Katumbi na ya Felix Tshisekedi

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mgawanyiko zaidi wa kisiasa unashuhudiwa kati ya mwanasiasa, Moise Katumbi na muungano wa siasa wa rais Felix Thisesekedi wa Sacred Union.

Moise Katumbi muda mchache baada ya mkutano wake na Rais Félix Tshisekedi tarehe 7 Novemba 2021.
Moise Katumbi muda mchache baada ya mkutano wake na Rais Félix Tshisekedi tarehe 7 Novemba 2021. © Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa sasa, kumeshuhudiwa mivutano ya kisiasa kati ya watu wa karibu wa Katumbi, Gavana wa zamani wa Katanga na wale wanaomzunguka rais Tshisekedi. 

Wiki iliyopita, Augustin Kabuya, kiongozi wa mpito wa chama cha rais Tshisekedi cha UDPS, kinachounda muungano huo, alinukuliwa akisema Katumbi na watu wake waondoke kwenye muungano huo. 

Hata hivyo, ripoti za ndani zinasema tofauti kati ya kambi hizi mbili zimekuwa zikishuhudiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, tangu kutajwa kwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguz CENI, Denis Kadima  ambaye alipingwa na Katumbi na kundi lake. 

Aidha, kundi la Katumbi limekuwa likidai kutengwa wakati wa mikutano muhimu ya kimkakati inayohusu muungano huo, ikiwa ni pamoja na wanadani wake aliowapendekeza katika Baraza la Mawaziri akiwemo Waziri wa Elimu Muhindo Nzangi, kumgeuka na hata kuunda chama chake, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.