Pata taarifa kuu

Namibia yataka kujadili upya mpango wa mauaji ya kimbari na Ujerumani

Namibia metangaza Alhamisi, Oktoba 27, 2022, kwamba ilikuwa imeitaka Ujerumani kujadili upya makubaliano kuhusu mauaji ya kimbari ya Herero na Namas yaliyofikiwa kati ya serikali hizo mbili.

Fuvu la kichwa cha binadamu, la watu wa Herero au Nama, likionyeshwa wakati wa sherehe mjini Berlin, Agosti 29, 2018.
Fuvu la kichwa cha binadamu, la watu wa Herero au Nama, likionyeshwa wakati wa sherehe mjini Berlin, Agosti 29, 2018. REUTERS - CHRISTIAN MANG
Matangazo ya kibiashara

Mnamo 2021, Berlin ilikiri kufanya mauaji ya halaiki nchini Namibia wakati wa ukoloni, kati ya mwaka 1884 na mwaka 1915, na kuahidi kulipa euro bilioni moja kama msaada.

Msaada huu ndio ambao tangu wakati huo umekuwa kiini cha mabishano. Ujerumani ilikiri kufanya mauaji ya kimbari wakati wa ukoloni, lakini haijajitolea kulipa fidia. Hata hivyo, hivi ndivyo wazao wa Waherero na Namas, makabila mawili yanayohusika na mauaji haya ya kimbari, ambayo yanadai zaidi ya wahanga 70,000 waliuawa.

Bilioni hii ya euro iliyoahidiwa kwa miaka thelathini ni katika mfumo wa msaada wa maendeleo: katika "kutambua mateso makubwa waliyopata wahanga" na kusaidia "ujenzi na maendeleo", kulingana na Berlin.

Familia zimekuwa zikipigania kwa miaka mingi kupata fidia halisi. Mapambano pia yamebebwa na upinzani wa kisiasa.

Shinikizo hili lilisababisha mijadala katika Bunge la Namibia, hasa ilipohitajika kuthibitisha mkataba huu. Kwa hiyo Namibia na Ujerumani zimeanzisha upya majadiliano. Mamlaka ya Windhoek ilitoa mapendekezo mapya mwezi Julaimwaka huu, Berlin lazima sasa kuyajibu. Suala zima ni iwapo neno "fidia" litakuwa katika rasimu mpya ya makubaliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.