Pata taarifa kuu

Biden awasili Misri kwa mkutano wa COP27 Sharm el Sheikh

Rais wa Marekani Joe Biden yupo nchini Misri, kuhudhuria mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi COP 27 kuelekezea mchango wa nchi yake, katika harakati za kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi. 

Rais wa Marekani Joe Biden akutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, mjini Sharm el-Sheikh, Misri, Novemba 11, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden akutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, mjini Sharm el-Sheikh, Misri, Novemba 11, 2022. via REUTERS - EGYPTIAN PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Rais Joe Biden muda huu anazungumza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 27 maarufu kama COP 27 unaofanyika huko nchini Misri, kutafuta mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi na kusema, dunia ipo kwenye hatari kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa. 

Awali Ikulu ya Marekani imesema hotuba ya rais Biden itatuama kwenye kufafanua juhudi ambazo Washington inachukua ili kupunguza utoaji wa gesi ya Kaboni na kuzisaidia nchi masikini kupambana na Mabadiliko ya Tabia nchi. 

Wajumbe wa mkutano huo wanataraji uwepo wa rais Biden utaongeza nguvu katika kusukuma malengo ya dunia ya kudhibiti kupanda kiwango cha joto kupindukia nyuzi 1.5 katika kipimo cha Celsius.

Mbali na mkutano huo rais Biden anakutana na rais Abdel Fattah al-Sisi kujadili hali ya haki za binadamu nchini humo, wakati huu nchi yake ikieleza kuguswa na hatua ya kuendelea kuzuiliwa kwa mwanaharakati mwenye uraia wa Uingereza na Misri, Alaa Abdel Fattah, ambaye amekuwa katika mgomo wa kula na kunywa tangu kuanza kwa mkutano wa COP27. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.