Pata taarifa kuu

DR Congo: Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23 yaahirishwa

Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na makundi ya waasi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia leo jijini Nairobi, yameahirishwa hadi mwishoni mwa juma hili, huku marais wa Rwanda Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wakitajiwa kukutana jijini Luanda huko Angola siku ya Alhamisi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto), washtumiana kila mmoja kutaka kuhatarisha usalama katika nchi ya mwingine.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto), washtumiana kila mmoja kutaka kuhatarisha usalama katika nchi ya mwingine. © AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Ingawa sababu za kuahirishwa kwa mazungumzo ya amani ya Nairobi kutowekwa wazi, tarifa zinasema, kuzuka kwa mapigano yanayoendelea katika maeneo ya mashariki mwa DRC kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23, lakini pia msimamo wa serikali ya Kinshasa kutokubali kukaa meza moja ya mazungumzo na waasi hao inayowaita magaidi, huenda ikawa ndio sababu za kuahirishwa kwa mazungumzo hayo. 

Kenya inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo  hayo, siku chache baada ya kuanza kutuma wanajeshi wake, kayika kikosi cha pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuwakabili waasi, iwapo juhudi za kidiplomasia hazitozaa matunda. 

Katika hatua nyingine, mkutano mwengine ambao pia ulikuwa ufanyike hivi leo huko jijini Luanda Angola na ambao ulikuwa Uwakutanishe marais wa Rwanda Paul Kagame, mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi chini ya msuluhishi wa nchi za Maziwa Makuu rais Joao Laurenso, na ambao pia ungelihudhuriwa na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika mashariki rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye Sasa umepangwa kufanyika siku ya Alhamis wiki hii. 

Haya yanajiri wakati huu waasi wa M23 wakiendelea kupambana na wanajeshi wa DRC na kusababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.