Pata taarifa kuu

Mchakato wa Nairobi wa kurejesha amani mashariki mwa DRC kuanza Nairobi

Mchakato wa Nairobi wa kurejesha amani mashariki mwa DRC unaanza tena Jumapili hii, Novemba 28 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mnamo Novemba 2, Rais wa Kenya William Ruto alitangaza kwamba atatuma kikosi cha wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mnamo Novemba 2, Rais wa Kenya William Ruto alitangaza kwamba atatuma kikosi cha wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. © AP/Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Makundi yenye silaha, wakuu wa kimila na viongozi wa mashirika ya kiraia wanatarajia kushiriki katika duru ya tatu ya mazungumzo haya.

Ajenda ya majadiliano haya bado haijatangazwa.

Katika mpango wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC), mkutano huu uliamuliwa mwezi wa Aprili mwaka huu katika mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi mjini Nairobi.

Awamu ya kwanza ya mazungumzo haya ilifanyika kuanzia Aprili 23 hadi 27 jijini Nairobi.

Wajumbe kutoka makundi 18 yenye silaha yaliyoko katika miko ya Kivy Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri walishiriki katika vikao vilivyosimamiwa na rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyata, wakiwepo waangalizi kutoka Rwanda, Uganda, Burundi, Umoja wa Mataifa, ICGLR, Marekani na Ufaransa.

Wakati wa hatua ya pili ya mwezi Mei mwaka huu, ujumbe wa pamoja kutoka ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ubalozi wa Kenya ulikwenda Goma, Bukavu, Beni na Bunia kwa mashauriano zaidi, miongoni mwa mengine, na viongozi wa jamii kutoka Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri.

Novemba 14 mwaka huu, alipokuwa Kinshasa, Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, mwezeshaji wa EAC wa mchakato wa Nairobi, pia alishauriana na wawakilishi wa mashirika ya kiraia na jamii tofauti za mikoa hii mitatu ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.