Pata taarifa kuu
UCHUMI-HAKI

Mahakama ya Angola yaamuru kuzuiwa kwa mali ya Isabel dos Santos nje ya nchi

Mahakama ya Juu ya Angola imeamuru kufungiwa kwa akaunti za benki na mali katika kampuni kadhaa zinazomilikiwa na Isabel dos Santos kwa jumla ya dola bilioni moja, kulingana na agizo la Desemba 19, lililowekwa wazi na kusainiwa na Jaji Daniel Modesto Geraldes.

Isabel dos Santos, 49, ni binti wa Rais wa zamani José Eduardo dos Santos, ambaye aliiongoza Angola kutoka 1979 hadi kustaafu kwake mnamo 2017.
Isabel dos Santos, 49, ni binti wa Rais wa zamani José Eduardo dos Santos, ambaye aliiongoza Angola kutoka 1979 hadi kustaafu kwake mnamo 2017. MIGUEL RIOPA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mali zilizozuiwa zinafikia dola za kimarekani bilioni moja. Mamlaka inabaini mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya rushwa.

Kampuni nyingi kati ya hizi ziko nje ya nchi, kama vile Msumbiji, Cape Verde na Sao Tome na Principe.

Mahakama imeamuru kuzuiwa kwa 70% ya hisa za kampuni ya mawasiliano ya MSTAR ya Msumbiji, 100% ya hisa za UNITEL T+, nchini Cape Verde, na UNITEL STP, huko Sao Tome na Principe, ambapo Isabel dos Santos ni "mwanahisa mkuu." ".

Makampuni mengine yaliyolengwa na agizo hilo la mahakama ni EMBALVIDRO, ambayo mahakama iliamuru kuzuiwa kwa 100% ya hisa na akaunti zote za benki; 70% ya hisa za UPSTAR Comunicação; na 100% ya hisa za UNITEL International Holding na UNITEL International.

Katika hati yenye kurasa 28, mahakama inaeleza jinsi fedha za SONANGOL, kampuni inayomilikiwa na serikali inayohusika na udhibiti wa mafuta, zilitumika kufadhili kampuni zinazomilikiwa na Isabel dos Santos.

Pia kulingana na mahakama, mrabaha ambao ulipaswa kulipwa kwa nchi ya Angola haukupitia kamwe mikononi mwa Hazina ya taifa.

Mbali na kunasa kwa dola bilioni 1, "uharibifu wenye thamani ya dola 1,136,996,825.56 ulipatikana katika kesi zingine za jinai," lakini pesa hizo hazijashughulikiwa na agizo hili.

Haijulikani ni jinsi gani mamlaka ya mahakama ya Angola inakusudia kutekeleza agizo la kufungia makampuni yenye makao yake makuu Msumbiji, Cape Verde na Sao Tome na Principe.

Agizo la mahakama linasema mwendesha mashtaka ameomba kuzuiwa kwa dola bilioni moja za Marekani chini ya sheria ya Angola na "Ibara ya 31 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa".

Isabel dos Santos, 49, ni binti wa Rais wa zamani José Eduardo dos Santos, ambaye aliiongoza Angola kutoka 1979 hadi kustaafu kwake mnamo 2017. Alifariki mnamo Julai 8 huko Barcelona, ​​​​nchini Uhspania. Mrithi wake, Rais wa sasa João Lourenço, amefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa kipaumbele chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.