Pata taarifa kuu
IVORY COAST- SIASA

Charles Ble Goude anatamani kuiongoza Ivory Coast

Charles Ble Goude, moja ya watu waliokuwa washirika wa karibu wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amesema anatamani siku moja awe kiongozi wa taifa hilo, matamshi anayoyatoa miezi michache tangu arejee nyumbani baada ya kufutiwa mashtaka na mahakama ya ICC.

Charles Blé Goudé mwansiasa nchini Ivory Coast
Charles Blé Goudé mwansiasa nchini Ivory Coast AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Goude ambaye alikuwa kitovu cha vurugu za mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2011, anatajwa kama moja ya watu wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wa taifa hilo.

“Kwa sasa sina ushirikiano na chama chochote nina fahamu vigogo wa siasa na nina waheshimu na mimi ni mgeni ila natazama tu,sina mgogoro na rais Gbagbo, huko Hague nilimhudumia kama mtoto wake.” Amesema Charles Ble Goude

Charles Ble Goude ni mwanasiasa mwenye umaarufu sana nchini Ivory Coast baada ya kufikishwa katika mahakama ya The Hague Uholanzi na ambapo alikamatawa baada ya mchafuko ya mwaka wa 2010 baada ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.