Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Shambulio la bomu kanisani: Islamic state yakiri kuhusika

Kundi la Islamic State nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limekiri kuhusika katika shambulio la bomu la hapo jana ambapo lililenga kanisa moja mashariki mwa nchi hiyo ambapo watu 10 waliuawa.

 Wanajeshi wa FARDC wakipiga doria
Wanajeshi wa FARDC wakipiga doria © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama kwenye mji wa Kisindi, watu wengine 39 walijeruhiwa katika moja ya shambulio ambalo limetajwa kuwa la kigaidi.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mawasiliano, waasi wa ADF wenye uhusiani na Islamic State ndio wanatajwa kuhusika na kwamba tayari msako umeanza dhidi ya waliotekeleza shambulio la hapo jana.

Kutokana na shambulio hilo, raia mashariki mwa nchi hiyo wameendelea kutoa mwito kwa Serikali kuwahakikishia usalama, hawa hapa ni baadhi ya manusura wa tukio la jana.

“Viongozi wetu watusaidia, wafanye uchunguzi ili hili jambo lisitokee tena.” amesema mmoja wa raia wa mashariki mwa DRC.

Kundi la ADF ni moja kati ya makundi hatari zaidi nchini DRC, kati ya makundi mengine zaidi ya 100 yanayofanya shughuli zao mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi hili limetajwa katika ripoti mbalimbali za kimataifa, kuhusika na mauaji ya mamia ya raia wa DRC pamoja na kutekeleza mashambulio ya kigaidi nchini Uganda, ambapo kwa sasa jeshi la Serikali na lile la Uganda wanaendesha operesheni ya pamoja dhidi ya ADF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.