Pata taarifa kuu
DRC- UGANDA- USALAMA

Uganda: Usalama umeimarishwa kwenye mipaka na DRC

Vyombo vya usalama nchini Uganda, hivi leo vimewekwa katika hali ya tahadhari hasa kwenye mipaka ya nchi hiyo na DRC, baada ya wanajihadi wa kiislamu kutekeleza shambulio kulenga kanisa.

Wanajeshi wa Uganda karibu na mpaka wa DRC
Wanajeshi wa Uganda karibu na mpaka wa DRC Photo: AFP Photo/Peter Busomoke
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa hatua zilizotangazwa na serikali ya Uganda ni pamoja na kuizuia safari za usiku za magari ya mizigo na zile za majini kutoka DRC, pamoja na kuimarishwa kwa doria.

Brigedia Jenerali Felix Kulaigye ni msemaji wa jeshi la Uganda.

“Karibu na sikukuu nadhani ilikuwa tarehe 24 tulimkamata jambazi wa ADF akiwa tayari na bomu upande wa Masaka kwa hivyo sisi tumekuwa waangalifu kutokana na vitendo vyao.” ameeleza Felix Kulaigye.

Tangu mwaka uliopita, jeshi la Uganda limeingia DRC kuwasaka waasi wa ADF wenye uhisiano na Islamic State, baada ya kufanya shambulio jijini Kampala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.