Pata taarifa kuu
HAKI-MAANDAMANO

Misri: Mawakili wasitisha mgomo wa kitaifa baada ya ushindi

Wanasheria wa Misri walisitisha mgomo wa kitaifa siku ya Jumapili Januari 22 wakipinga kuhukumiwa kwa wenzao sita kifungo cha miaka miwili jela na mahakama ya Marsa-Matrouh, kaskazini-magharibi mwa Misri, kwa kugombana na makarani. Mahakama ya Rufaa iliamua kuwaachilia mawakili hao wakisubiri kesi mpya Februari 5.

Mgomo wa kitaifa ambao ulisababisha kuachiliwa kwa wanasheria wa Marsa-Matrouh ni kielelezo cha mapambano ya chama hiki katika nchi ambayo vyama vingi vya wafanyakazi huepuka kufanya maandamano.
Mgomo wa kitaifa ambao ulisababisha kuachiliwa kwa wanasheria wa Marsa-Matrouh ni kielelezo cha mapambano ya chama hiki katika nchi ambayo vyama vingi vya wafanyakazi huepuka kufanya maandamano. © mizan
Matangazo ya kibiashara

Mgomo wa kitaifa ambao ulisababisha kuachiliwa kwa wanasheria wa Marsa-Matrouh ni kielelezo cha mapambano ya chama hiki katika nchi ambayo vyama vingi vya wafanyakazi huepuka kufanya maandamano.

Hata kama mgomo unaruhusiwa na Katiba, hakuna mtu anayeweza kuutumia kwa kuhofia athari na sheria za kipekee zinazowezesha mtu kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka.

Lakini chama cha wanasheria kimeendelea kutii utamaduni wake wa uhuru chini ya marais waliotangulia nchini Misri, iwe wametoka katika safu ya jeshi au Muslim Brotherhood.

Siku ya Jumamosi, mawakili waliandamana mbele ya makao makuu ya chama chao na kulaani "nguvu ya kuwachinja". Mnamo Desemba, wanasheria pia waliandamana dhidi ya kuanzishwa kwa ankara ya kielektroniki kwa hatua zote za kisheria, ambazo huongeza gharama kwa wateja wao.

Uwezo wa mawakili wa kuzorotesha mfumo wa mahakama kwa kugoma unafaa zaidi kwani mahakama za Misri zimezidiwa na zaidi ya kesi milioni 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.