Pata taarifa kuu
UGANDA- CHINA- MAFUTA

Uganda yazindua uchimbaji wa mafuta utakaosimamiwa na kampuni ya China

Uganda imezindua uchimbaji wa mafuta utakaosimamiwa na kampuni ya China, katika kisima chake cha kwanza kati ya vinne, katika mradi wake mkubwa wa kuanza kuzalisha mafuta, kuelekea mwaka 2025 ambapo nchi hiyo imepanga kuanza kusafirisha bidhaa hiyo katika soko la kimataifa.

Uganda imezindua uchimbaji wa mafuta utakaosimamiwa na kampuni ya China
Uganda imezindua uchimbaji wa mafuta utakaosimamiwa na kampuni ya China © Government of Uganda
Matangazo ya kibiashara

Kisima hicho kinachopatikana karibu na Ziwa Albert, kinatarajiwa kuzalisha mapipa 230,000 ya mafuta ghafi kwa siku.

Rais Yoweri Museveni amesema mradi huo ni salama, licha ya pingamizi kutoka kwa wanaharakati wa mazingra.

“Mafuta haya si tatizo hata kidogo maana hewa aina hii aina ya ukaa ambayo inatokana na nishati ya mafuta sio tatizo.” ameeleza rais Museveni.

Mapema leo mpinzani wake wa kisiasa Kizza Besigye aliyekuwa ameandaa mkutano kujadili suala hili la mafuta nchini humo, alizuiwa na maafisa wa usalama jijini Kampala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.