Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema hatojiuzulu siasa

NAIROBI – Licha ya shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa mrithi wake, aliyekuwa rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amesema hatojiuzulu siasa na kwamba kiongozi wake wa chama ni kinara wa upinzani Raila Odinga.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga wakati wa kampeni mwaka wa 2022, jijini Nairobi.
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga wakati wa kampeni mwaka wa 2022, jijini Nairobi. © THOMAS MUKOYA/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Kenyatta, yanategua kitendawili kuhusu ushiriki wake kisiasa, wakati huu shinikizo likitolewa na wandani wa rais Ruto, asilipwe mafao yake kama ataendelea na siasa.

Maimuna Mwidau, ni mchambuzi wa siasa za Kenya, akiwa jijini Nairobi.

“Kauli ya rais kwanza imewachukua wengi kwa mshtuko kwa sababu amezungumza kama mtu amabye ameshajipanga.”amesema Maimuna Mwidau

Kiongozi huyo wa chama tawala cha zamani cha Jubilee ameendelea kusisitiza kuwa anagali anamuunga mkono kinara wa chama cha upinzani nchini humo mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, wikendi iliyopita akionekana katika mkutano wa hadhara katika eneo la magharibi ya Kenya akiandamana naye Odinga.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.