Pata taarifa kuu
UGANDA- HAKI ZA BINADAMU

Ofisi ya haki ya UN inataka kusalia Uganda licha ya kutakiwa kuondoka

NAIROBI – Tume ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia masuala ya Haki za binadamu imesema ipo kwenye mazungumzo na serikali ya Uganda, baada ya kutakiwa kufunga Ofisi yake jijini Kampala.

Volker Turk, Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa UN
Volker Turk, Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa UN AP - Marwan Ali
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, mwanasiasa wa upinzani, Bob Wine, ameikashifu tume ya haki za binadamu nchini humo, kwa kushindwa kusimamia ukweli kuhusu kutekewa kwa wafuasi wake. Hapa anazungumzia mmoja wa wafuasi wake aliyekamatwa na kuteswa.

“Tunaendelea kudai kuachiliwa kwa wale wanaoshikiliwa kinyume cha sheria.” amesema Bobi Wine.

Maofisa wa polisi nchini humo nao wamekana madai ya Bobi Wine kuwa walimkamata na kumtesa mfuasi wake. Kiongozi huyo wa upinzani amekuwa akiituhumu serikali kwa kuwakandamiza wafuasi wake na kutatiza mikutano yake ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.