Pata taarifa kuu

Ufaransa kutoingila miradi ya TotalEnergies nchini Uganda

NAIROBI – Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya biashara za nje, Olivier Becht, amesema kwa sasa Serikali haitoi ufadhili kwa makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa mafuta na gesi, na kwamba haiingilii operesheni za makampuni binafsi katika uwekezaji wa nishati zenye utata.

Olivier Becht -Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya biashara za nje
Olivier Becht -Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya biashara za nje © RFI
Matangazo ya kibiashara

Becht, amesema haya wakati akijibu swali kuhusu msimamo wa Ufaransa kuhusu mradi wa ujenzi wa homba la mafuta kutoka Uganda kwenda Tanzania, mradi ambao bunge la Ulaya lilipiga kura kutaka usitishwe, kwa hofu ya uchafuzi wa mazingira na ripoti za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa utekelezaji wake.

“Mnajuwa serikali haipo kwa ajili ya kutuhumu miradi ya makampuni binafsi, swala ni kwamba je tunawasaidia kifedha? Jibu ni kwamba hapa.”amehoji Olivier Becht.

Uganda na Tanzania zinajenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima mpaka bandari ya Tanga, mradi unaojengwa na kampuni ya mafuta ya TotalEnergies ya Ufaransa na kampuni ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.