Tanzania yaidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta Afrika Mashariki
NAIROBI β Serikali ya Tanzania, imeidhinisha kujengwa kwa bomba la mafuta la Afrika Mashariki lenye thamani ya Dola Bilioni 3.5 kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, licha ya mradi huo kukosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu na wale wa mazingira.
Imechapishwa:
Cheza - 00:37
January Makamba ni Waziri wa Nishati nchini humo.
βMazingira hayataharibika ndio kwa kifupi hata unapojenga nyumba lazima uchimbe msingi, kama ni uharibifu utakaotokea ni kama ule ambao unatokea unapofanya mradi wowote.βameeleza January MakambaΒ Waziri wa Nishati nchini Tanzania.
Mwezi uliopita, Uganda ilitoa leseni kwa kampuni zitakazojenga bomba hilo, ikiongozwa na TotalEnergies ya Ufaransa.