Pata taarifa kuu

Uganda: Rais Museveni afanya mazungumzo na Zelensky wa Ukraine

NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara ya kwanza.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni © StateHouseUganda
Matangazo ya kibiashara

Uganda ambayo ni mshirika wa karibu wa Urusi, tangu kuanza kwa mzozo unaoshuhudiwa, amekuwa akioneka kutoegemea upande wowote.

Waziri wa anayehusika na uhusiano wa kimataifa Henry Okello Oryem, anaelezea walichozungumza viongozi hao wawili.

“ilikuwa ni mwito kutoka kwa mkuu wa nchi ya Ukraine kwa rais Museveni kujaribu kuhimiza Uganda kubadili msimamo wakati itakapopiga kura katika baraza la usalama la umoja wa mataifa wakati wa kumbukumbu ya vita vya Urusi na Ukraine kuanza.” ameeleza Henry Okello Oryem

Vita hivyo vya ukraine vimesbabisha tofauti za kisiasa miongoni mwa mataifa ya Afrika, nchi kama Eriterea, Mali na Jamhuri ya Africa ya kati zikiunga mkono uvamizi huo, mengine yakilaani uvamizi huo huku mengine yakionekana kutounga mkono upande wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.