Pata taarifa kuu

Rais Kiir awataka wakimbizi wanaoishi nje ya nchi kurejea nyumbani

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anawataka raia wa nchi yake zaidi ya Milioni 2, wanaoishi katika mataifa ya Kenya, Uganda na Misri, kuanza kurudi nyumbani, na kuwaahidi kuwa serikali yake itawapa usalama.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Juba, Sudan Kusini, Julai 9, 2021. (Picha na Peter Louis GUME / AFP)
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Juba, Sudan Kusini, Julai 9, 2021. (Picha na Peter Louis GUME / AFP) AFP - PETER LOUIS GUME
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza akiwa jijini Juba siku ya Jumatano, Kiir amesema kuwarejesha nyumbani wakimbizi hao ni ajenda muhimu katika serikali yake.

Serikali itawapa ulinzi wakimbizi wote watakaorudi nyumbani kwa hiari yao, na tutashirikiana na wadau wa kimataifa kuhakikisha kwamba mpango huu umetekelezwa ipasavyo ili wakimbizi hao waanze maisha mapya, wasio na makao ninawahakikishia mtakuwa na makao mapya. Amesema Kiir.

Kwenye mkutano na wawakililishi wa wakimbizi nchini humo, rais Kiir amesema serikali yake pia ina lengo la kuwapa makazi wakimbizi wa ndani kwa ndani, lakini sio lazima wapewe makazi katika sehemu walizotoka.

Raia wengi za Sudan Kusini, wameikimbia nchi yao kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2013, wakati majeshi ya Kiir yalikabiliana na yale ya kiongozi wa upinzani Riek Machar.

Nchi ya Sudan kusini iliyojinyakulia uhuru mwaka 2011, bado haijatekeleza kikamilifu mkataba wa amani wa mwaka 2018, kwa kuwa baadhi ya sehemu nchini humo bado zinashuhudia ghasia za mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.