Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Bamako yaonya dhidi ya vitisho kwa makubaliano muhimu ya amani

Wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali wameionya vikali Algeria na baadhi ya washirika wa kimataifa dhidi ya vitisho vya makubaliano makubwa ya amani na makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo, katika barua ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Jumatano.

Waziri Mkuu wa Mali Choguel Maïga (kushoto) akiwa pamoja na rais wa mpito Assimi Goïta, hapa ilikuwa huko Kati, Januari 20, 2022.
Waziri Mkuu wa Mali Choguel Maïga (kushoto) akiwa pamoja na rais wa mpito Assimi Goïta, hapa ilikuwa huko Kati, Januari 20, 2022. AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika utawala wa kijeshi, Kanali Meja Ismaël Wagué, anamshutumu mmoja ya makundi yaliotia saini, CMA, muungano wa makundi yenye wafuasi wengi wa Tuareg wanaotaka kujitenga na kujitawala, kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Makubaliano ya Algiers ya 2015, mwaka huu katika barua ya tarehe 24 Februari iliyotumwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra.

Mamlaka ya Mali inaenda mbali na kuhoji uaminifu wa upatanishi wa kimataifa unaounga mkono utekelezwaji wa makubaliano haya. Algeria ndiye kiongozi wa upatanishi huu unaoleta pamoja Umoja wa Mataifa, mashirika ya Afrika na washirika wa kigeni.

"Tabia ya baadhi ya mienendo ni kikwazo kwa amani," amesema waziri. Anaishutumu CMA kwa "ushirikiano wa wazi unaoongezeka na makundi ya kigaidi". "Serikali, ikiwa imeshikamana na utekelezaji wa makubaliano ya busara, itakataa moja kwa moja tuhuma yoyote ambayo inaweza kuwajibika kwa matokeo ya ukiukaji (wake)", anaonya.

Onyo hili linakuja wakati wa mvutano mkubwa kati ya wanajeshi waliochukua madaraka kwa nguvu mnamo 2020 huko Bamako na makundi yaliyotia saini kwenye makubaliano ya Algiers, CMA ikiwa mstari wa mbele. Shaka inaongezeka juu ya mustakabali wa makubaliano.

Mkataba huo uliotiwa saini mwaka 2015 na serikali ya Mali na makundi yanayojumuika na CMA ulikomesha uhasama ulioanza na uasi wa Kisalafi 2012 kaskazini mwa nchi. Wanajihadi wanaendelea kupigana na mzozo wa usalama umeenea hadi katikati mwa Mali na pia katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger.

Mkataba wa 2015 unawasilishwa na upatanishi wa kimataifa kama muhimu kwa utulivu wa nchi iliyo katika machafuko. Lakini imekuwa katika hali mbaya kwa miaka kadhaa. CMA ilitangaza mwezi Desemba kuwa inasitisha ushiriki wake katika utekelezaji wake. Mnamo mwezi Februari afisa anayeunga mkono jeshi alitabiri kuanza tena kwa uhasama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.