Pata taarifa kuu

Museveni na Ramaphosa wajadili usalama wa mashariki ya DRC

NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye amekuwa ziarani nchini Afrika Kusini na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Cyril Ramaphosa, wamezungumzia usalama wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuahidi ushirikiano kuyashinda makundi ya waasi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni © StateHouseUganda
Matangazo ya kibiashara

“Jeshi la Afrika Kusini limekuwa huko nasi pia tupo, lilikuja wakati waasi wa M23 walipouuteka mji wa Goma nasi tumekuja kwa sababu kuna changamoto mingi sana huko kuna M23 na makundi mengine.”ameeleza rais Museveni.

Wanajeshi wa Uganda ni miongoni mwa wale wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, waliotumwa nchini DRC, haswa katika eneo la mashariki kupambana na makundi ya waasi nchini humo wakiwemo M23, ADF na makundi mengine.

Kwa muda sasa, raia wa eneo hilo wamekuwa wakitatizwa na mashambulio yanayotekelezwa na makundi ya waasi, wengi wakiripotiwa kuyahama makazi yao kwa hofu ya kusahmbuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.