Pata taarifa kuu

Marekani yasisitiza amani nchini Ethiopia huku ikitoa msaada wa kibinadamu

NAIROBI – Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, ambaye amekuwa ziarani nchini Ethiopia, ameitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha kuwa wale waliohusika na mzozo wa jimbo la Tigray, wanawaajibishwa na kuhakikisha kuwa amani iliyorejea inadumu.

Antony Blinken, waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani
Antony Blinken, waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani AP - Stefani Reynolds
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ametangaza msaada wa Dola Milioni 331 kusaidia kupatikana kwa misaada ya kibinadamu nchini humo.

“Tumejitolea kwa huu ushirikiano na Ethiopia, tunatekeleza jukumu letu kuhakikisha kwamba raia wanapata kile wanahitaji.”ameeleza Anthony Blinken.

Blinken aidha ameeleza kufurahishwa na hatua ya Marekani kuwa katika mstari wa mbele kutoa msaada wa chakula ambapo kila siku nchi yake inatoa msaada wa asilimia 50 katika mpango wa chakula.

Blinken vile vile ameeleza kuguswa na  kujitolea kwa viongozi na watetezi wa haki za binadamu huko nchini Ethiopia akikaribisha  juhudi zao za kuunga mkono mazungumzo ya pamoja kuhakikisha kuwa usalama unadumu nchini humo.

Nchini Ethiopia, Marekani inatoa  zaidi ya dola za Mareakani  milioni 331 kama msaada wa  kibinadamu ili kusaidia huduma za afya na lishe, upatikanaji wa maji safi, kukabiliana na ukosefu wa chakula, na kutoa huduma muhimu kwa wakimbizi.

Blinken ambaye yupo ziarani barani Afrika, anatembelea nchi ya Niger hivi leo Alhamis.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.