Pata taarifa kuu

Angola: Bunge limeidhinisha kutumwa kwa wanajeshi wake 500 DRC

NAIROBI – Bunge la Angola, hivi leo limeidhinisha kutumwa kwa wanajeshi wake 500 kwenda nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya waasi na serikali ya DRC ambayo yaliratibiwa na Luanda, kuvunjika.

João Lourenço rais wa Angola na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi
João Lourenço rais wa Angola na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi © Facebook Presidência de Angola
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hawa watatumwa nchini Congo kwa muda wa mwaka mmoja.

Kwa mujibu kiongozi wa shughuli za Bunge, wabunge wote 178 kati ya 220 waliokuwepo, walipiga kura ya ndio kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao nchini DRC.

Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani, Francisco Furtado, Luanda itatuma kati ya wanajeshi 450 hadi 500 na kwamba watahudumu nchini humo kwa muda wa miezi 12.

Tangazo la Angola kutuma wanajeshi wake nchini Congo, kwa mara ya kwanza lilitolewa na rais Joao Lourenco, ambaye alisema lengo litakuwa ni kutwaa maeneo yanayokaliwa na waasi wa M23 pamoja na kutoa usalama kwa raia.

Serikali ya Luanda, inasema uamuzi wa kutumwa kwa wanajeshi hawa ulifanyika baada ya majadiliano na utawala wa Kinshasa, na kwamba tayari viongozi wa ukanda na wale wa umoja wa Mataifa, wanataarifa.

Uamuzi huu umechukuliwa saa chache kabla ya rais Felix Tshisekedi kufanya ziara jijini Luanda, hapo kesho ambapo atakuwa na mazungumzo zaidi na mwenyeji wake rais Lourenco.

Nchi ya Angola, imejihusisha pakubwa katika juhudi za upatanishi kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23, ambapo licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano, waasi hao wamezidisha mashambulizo dhidi ya vikosi vya Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.