Pata taarifa kuu

Wafanyakazi wawili wa ICRC waliotekwa nyara mapema Machi waachiliwa nchini Mali

Wafanyakazi wawili wa Shirika la Kimataifa la Msalaba na Ilani Nyukundu (ICRC) waliotekwa nyara wiki mbili zilizopita kaskazini mwa Mali wameachiliwa "salama salimini na bila masharti", shirika hilo lisilo la kiserikali limetangaza usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Wafanyakazi wawili wa shirika la Kimataifa la Msalaba na Ilani Nyekundu nchini Mali wameachiliwa huru Jumapili jioni.
Wafanyakazi wawili wa shirika la Kimataifa la Msalaba na Ilani Nyekundu nchini Mali wameachiliwa huru Jumapili jioni. AFP PHOTO/Waakhe WUDU
Matangazo ya kibiashara

"Wafanyakazi wawili wa ICRC waliotekwa nyara mnamo Machi 4 kati ya (miji ya) Gao na Kidal (kaskazini) waliachiliwa (Jumapili) jioni hii," tawi la Mali la ICRC lilitangaza kwenye Twitter. "Wenzetu wanaendelea vizuri na wameachiliwa, wako salama salimini na bila masharti," shirika hilo limesema. ICRC 'inawashukuru wale wote waliochangia kuachiliwa kwao'.

Wafanyakazi hao wawili "wataunganishwa tena na familia zao haraka iwezekanavyo", ametangaza Antoine Grand, mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Mali, katika taarifa iliyochapishwa hata hivyo. ICRC inasisitiza kwamba haitafichua majina au uraia wa wafanyakazi hao wawili "kulinda usalama wao". Pia limesema halitatoa maelezo yoyote ya kuzuiliwa, kutekwa au kuachiliwa, kufuatia sheria inayozingatiwa katika mazingira hayo.

Mali imekumbwa na ghasia za kila aina na kuenea kwa wanajihadi tangu mwaka 2012. Nchi hii kubwa, maskini na isiyo na bahari imetumbukia katika mgogoro mkubwa, sio tu usalama, lakini pia kisiasa na kibinadamu. Inatawaliwa na jeshi kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi mnamo mwaka 2020 na 2021.

Vurugu hizo zinatekelezwa na makundi yenye silaha yenye mafungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State, lakini pia na watu wanaojiita wanamgambo na majambazi. Utekaji nyara ni kipengele kimoja cha vurugu hizi, ambazo zinalenga wageni au raia wa Mali. Misukumo, ya kiitikadi au ya kiovu, inategemea fidia hadi kitendo cha kulipiza kisasi kupitia utashi wa kujadiliana.

Kuendelea kwa shughuli

Ukosefu wa usalama hufanya kazi ya mashirika ya kibinadamu kuwa ngumu sana na hatari. Daktari kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Januari mashariki mwa Mali kabla ya kuachiliwa mwezi Februari. Nchini Mali, lakini pia kwingineko katika Sahel, mashirika ya misaada ya kibinadamu kwa kawaida yanashutumiwa kutumikia maslahi ya nje, ambayo wanayakanusha.

"ICRC ni shirika la kibinadamu pekee, na lisiloegemea upande wowote, huru na lisilopendelea," Shirika la Msalaba na ilani Nwekundu limesema katika taarifa yake. "Timu zake lazima ziheshimiwe na kulindwa. Vitendo kama hivyo vinahatarisha shughuli zozote za kibinadamu na vinaweza kuwa na athari kubwa katika huduma za kibinadamu zinazotolewa kwa watu walio hatarini zaidi," taarifa hiyo imeongeza.

"Tunataka kuendelea na shughuli zetu za kibinadamu kwa karibu iwezekanavyo na watu walioathiriwa na ghasia na mzozo nchini Mali huku tukihifadhi usalama wa wafanyakazi wetu katika eneo ambalo mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana," anasema Patrick Youssef, mkurugenzi wa shirika la ICRCkatika ukanda wa Afrika, akinukuliwa katika taarifa.

Mateka kadhaa, wa ndani au wa kigeni, wameshikiliwa katika Sahel, akiwemo mwandishi wa habari wa Ufaransa Olivier Dubois tangu 2021, Mmarekani Jeffery Woodke (2016), Muaustralia Arthur Kenneth Elliott (2016) na Mromania Iulian Ghergut (2015). Mhubiri wa Kijerumani, Padre Hans-Joachim Lohre, ambaye hajasikika tangu mwezi Novemba 2022, anaaminika kuwa alitekwa nyara nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.