Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Gwaride la kisiasa lapigwa marufu kabla ya uchaguzi wa urais wa Sierra Leone

Mamlaka nchini Sierra Leone imepiga wmarufuku gwaride la kisiasa la mitaani, mila kila wakati wa kampeni za uchaguzi katika nchi hii ya Afrika Magharibi, chini ya miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais.

Vipindi vya uchaguzi sio "wakati wa densi na furaha", lakini ni "wakati wa kutafakari zaidi", imesema Tume ya Udhibiti wa Vyama vya Siasa.
Vipindi vya uchaguzi sio "wakati wa densi na furaha", lakini ni "wakati wa kutafakari zaidi", imesema Tume ya Udhibiti wa Vyama vya Siasa. AP - Cooper Inveen
Matangazo ya kibiashara

Vipindi vya uchaguzi sio "wakati wa densi na furaha", lakini ni "wakati wa kutafakari zaidi", imesema Tume ya Udhibiti wa Vyama vya Siasa, taasisi ya serikali, katika taarifa ikitangaza ikitangaza marufuku hayo. Kawaida, wakati wa kampeni, vyama vikuu viwili-SLPP (madarakani), na APC huandaa gwaride kupitia miji mbalimbali nchini humo.

Sheria mpya sasa inavitaka vyama kuteua mahali pa kudumu (uwanja, kituo cha jamii ...) kufanya mikutano yao ya kampeni. "Kuwasumbua raia wetu, wanasiasa, kwa miaka mingi, wametumika kama mizunguko ya mitaani ili kuvuruga tafakari ya wapiga kura, hasa vijana, kwa kutumia dawa za kulevya na vitu vingine vyenye ulevi," inaelezea Tume.

Kulingana na Lucien Momoh, msemaji wa Tume hiyo, marufuku hiyo inaweza kuifanya iwezekane "kupunguza vurugu". "Mwaka hadi mwaka nchini Sierra Leone, Gwaride la kisiasa la mitaani kwa ajili ya kampeni za uchaguzi zimekuwa tishio kubwa kwa usalama wa raia wa kawaida, "ameliambia shirika la habari la AFP. "Mikutano hii iliharibiwa na vurugu na matusi na vitisho kwa wapinzani wa kisiasa."

Uchaguzi wa urais, wa wabunge na wa serikali za mitaa katika nchi hii yenye wakaazi milioni 8 utafanyika Juni 24. Rais Julius Maada Bio atawania muhula wa pili. Mpinzani wake mkuu, kiongozi wa chama cha APC Samura Kamara, kwa sasa anakabiliwa na kesi ya ufisadi. Ikiwa atahukumiwa, hataweza kuwania katika uchaguzi au kushikilia wadhifa wowote ndani ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.