Pata taarifa kuu
RUSHWA-HAKI

Ubadhirifu nchini Equatorial Guinea: ni nani aliyeghushi saini ya Rais Obiang?

Waziri na waziri wa zamani wa Equatorial Guinea wanashukiwa kuhusika katika kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma wa "faranga za CFA bilioni kumi" (swa na euro milioni 15.2), televisheni ya serikali (TVGE) imetangaza siku ya Ijumaa.

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, pichani mwaka 2017, ndiye rais aliyekaa muda mrefu zaidi madarakabi barani Afrika.
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, pichani mwaka 2017, ndiye rais aliyekaa muda mrefu zaidi madarakabi barani Afrika. REUTERS - DAVID MERCADO
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo unalenga kundi la watu watano wa Equatorial Guinea walioanzisha kampuni kadhaa "hewa" tangu 2019, ili kupata kandarasi za umma, hasa kwa kughushi saini ya Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye anatawala nchi hii tangu mwaka 1979, na anashikilia rekodi ya dunia ya kuishi muda mrefu madarakani kwa mkuu wa nchi aliye hai, bila kuwajumuisha wafalme.

Watu hawa watano walikamatwa na wanazuiliwa katika kituo cha polisi huko Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea, nchi ya tatu kwa utajiri katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa Pato la Taifa kwa kila mtu (Benki ya Dunia, 2021), lakini imewekwa kwenye nafasi ya 172 kati ya nchi 180 duniani kwa rushwakatika ripoti ya shirika la kimataifa la Transparency International.

Watu hawa waliunda "kampuni hewa tisa" ambazo zilitoa huduma za matengenezo, majengo ya umma na matengenezo ya ufuo, kulingana na TVGE, ambayo inaongeza kuwa kampuni hizi zilihitimisha 'mikataba 24 ya uongo' na serikali.

TVGE inamtuhumu Rufino Ndong Esono Nchama, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Ukuzaji wa Ufundi tangu 2017, na Valentin Ela Maye, ambaye alikuwa Waziri wa Uchumi na Fedha kati ya mwaka 2020 na 2023, kwa kuwa 'katika malipo' ya makampuni haya hewa:.

Televisheni ya serikali inabainisha kuwa mahakama inatathmini uhusiano unaodhaniwa kuwa walikuwa nao na baadhi ya makampuni "ya uwongo", na inathibitisha kwamba watu hawa wawili muhimu kila mmoja alipokea faranga za CFA milioni tano kwa mwezi (sawa euro 7,600).

Ufunguzi wa uchunguzi huo ulmethibitishwa kwa shirika la habari la AFP na chanzo kinachofahamu faili hiyo ambacho kiliomba kutotajwa jina, kikibainisha kuwa wachunguzi bado wanajaribu kubaini idadi ya watu waliohusika. Kusikizwa mahakamani kwa Waziri Nchama kunahitaji idhini kutoka kwa Waziri Mkuu, imeripoti televisheni ya serikali. Ikihojiwa na shirika la habari la AFP, Wizara ya Sheria haikutaja aina ya mashtaka dhidi ya watu wanaoshukiwa, wala adhabu zilizotolewa dhidi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.