Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

Kinshasa yalishtumu jeshi la Rwanda na M23 kwa kuandaa mashambulizi dhidi ya Goma

Jeshi la DRC, FARDC,  limeshutumu rasmi vikosi vya ulinzi vya Rwanda (RDF) na waasi wa M23 kwa kuandaa mashambulizi dhidi ya mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo waasi wanadhibiti maeneo kadhaa licha ya kuwepo kwa majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jenerali Sylvain Ekenge, msemaji wa jeshi la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Novemba 5, 2022.
Jenerali Sylvain Ekenge, msemaji wa jeshi la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Novemba 5, 2022. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la DRC, Jenerali Sylvain Ekenge, amebaini kwamba harakati za jeshi la Rwanda na waasi wa M23 zinaendelea katika mkoa wa Kivu Kaskazini kwa lengo la "kushambulia mji wa Goma", amesema, kulingana na tovuti ya VOA, ikinukuu maafisa kadhaa.

"Tunashuhudia harakati za wanajeshi wa RDF na M23 na waajiri wao, ambao wamemaliza mafunzo nchini Rwanda na Tchanzu, ili kushikalia tena ngome zao za zamani huko Kibumba na Rugari, ambapo wameweka makao yao makuu," Jenerali Sylvain Ekenge amesema kwenye video, iliyotumwa kwa vyombo vya habari na idara ya mawasiliano ya ofisi ya msemaji huyo wa FARDC.

Kulingana na afisa huyo, lengo la kutumwa tena kwa wanajeshi hao wa Rwanda na waasi wa M23 ni "kushambulia mji wa Goma na kuzidisha mzozo wa kibinadamu na ukosefu wa usalama".

Kundi la waasi la M23 au serikali ya Rwanda haijasema chochote kuhusiana na madai haya ya jeshi la DRC, FARDC.

Serikali ya Kongo kupitia Waziri wake wa Ulinzi, Jean-Pierre Bemba, ilitangaza wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Alhamisi ya wiki iliyopita kwamba jeshi la Rwanda na waasi wa M23 walikuwa wakiimarisha ngome zao "kwa kutarajia mashambulizi ya jumla kwa "kudhibiti" mji wa Goma.

Mji huo una zaidi ya wakazi milioni moja, ambao wameongezwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutoka maeneo ya Nyiragongo na Rutshuru, kaskazini mwa Goma.

Rais wa DRC aonyooshea kidole cha lawama kikosi cha EAC

Ikishutumiwa kuunga mkono M23, Kigali imekuwa ikikanusha na kulishutumu jeshi la DRC kwa kushirikiana na waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Kikosi cha kijeshi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kinachojumuisha majeshi ya Kenya, Burundi, Sudan Kusini na Uganda kimetumwa tangu mwishoni mwa mwaka 2022 katika eneo hilo kuwapokonya silaha waasi wa M23.

Kinshasa inashutumu kikosi hiki cha kikanda kwa kutowajibi kwa jukumu lake na kuendelea kuwasiliana na waasi wa M23, isipokuwa kikosi cha Burundi.

Rais Félix Tshisekedi, aliye madarakani tangu 2019, hivi karibuni aliomba msaada wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo iliahidi kupeleka wanajeshi wake mara moja mashariki mwa DRC.

Wakuu wa EAC wakutana Bujumbura

Kikosi cha EAC kinaweza kuombwa kuondoka nchini DRC mwishoni mwa mwezi Juni, kulingana na rais wa DRC.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki utafanyika Jumatano hii mjini Bujumbura, Burundi kwa ajili ya Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hali ya usalama mashariki mwa DRC ni miongoni mwa mambo muhimu katika ajenda ya mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.