Pata taarifa kuu

Majengo ya Gazeti la uchunguzi yafungwa nchini Burkina Faso

Majengo ya Gazeti la uchunguzi la  L'Evénement nchini Burkina Faso yamefungwa na mamlaka kwa sababu ya mzozo wa kodi, uamuzi uliokanushwa Jumapili na Chama cha Wachapishaji wa Vyombo vya Habari Binafsi (SEP) ambacho kinalaani mamalaka "kuiingilia kazi za mamlaka ya kodi".

Kulingana na ripoti ya Reporters Without Borders (RSF) iliyochapishwa mwezi Aprili, ukanda wa Sahel ambao Burkina Faso ni sehemu yake unatishiwa kuwa "eneo kubwa zaidi la watu wasio na habari barani Afrika".
Kulingana na ripoti ya Reporters Without Borders (RSF) iliyochapishwa mwezi Aprili, ukanda wa Sahel ambao Burkina Faso ni sehemu yake unatishiwa kuwa "eneo kubwa zaidi la watu wasio na habari barani Afrika". AFP - ANNIE RISEMBERG
Matangazo ya kibiashara

"Makao makuu ya gazeti hilo yalifungwa Ijumaa asubuhi na idara ya ushuru," mkurugenzi wa uchapishaji wa gazeti la uchunguzi linalotoka mara mbili kwa mwezi, Atiana Serge Oulon, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Ni vigumu kutofanya uhusiano kati ya kazi ya gazeti hili la uchunguzi na kufungwa kwake kijeshi kwa kutumia kodi," SEP ilisema kwa masikitiko katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili. "Kutumika kwa mamlaka ya ushuru na huduma za umma kwa ujumla kunyamazisha sauti zinazopingana au kuwaadhibu wale wanaowazuia kwenda kwenye miduara ni kazi hatari na isiyo na tija ambayo lazima iachwe", iliongeza SEP.

Burkina Faso imekuwa ikiongozwa tangu Septemba na Kepteni Ibrahim Traoré, ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi, mapinduzi ya pili kwa kipindi cha mwaka mmoja. Mwishoni mwa mwezi Machi, serikali ya mpito ilihakikisha kwamba itasalia "kimsingi kushikamana" na uhuru wa kujieleza, siku chache baada ya kusitishwa kwa matangazo ya kituo cha France 24. Mapema mwezi Aprili, waandishi wa Magazeti ya kila siku ya Ufaransa Le Monde na Liberation walifukuzwa nchini Burkina Faso.

Tangu mwaka wa 2015, Burkina Faso imekumbwa na ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi wenye uhusiano na Islamic State na Al-Qaeda, ambayo yameua watu 10,000 kwa jumla - raia na wanajeshi - kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali, na takriban milioni mbili kukimbia makazi.

Kulingana na ripoti ya Reporters Without Borders (RSF) iliyochapishwa mwezi Aprili, ukanda wa Sahel ambao Burkina Faso ni sehemu yake unatishiwa kuwa "eneo kubwa zaidi la watu wasio na habari barani Afrika".

Vyombo vya habari vya ndani na kimataifa vimekuwa vikikabiliwa na "kuzorota mara kwa mara" kwa mazingira yake ya kazi kwa miaka kumi, inasema ripoti inayohusu Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger, Chad, lakini pia kaskazini mwa Benin, eneo linalokabiliwa na changamoto kama hizo za usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.