Pata taarifa kuu

Angola: Rais João Lourenço amfuta kazi waziri wa maendeleo ya uchumi na jamii

NAIROBI – Rais wa Angola João Lourenço amemfuta kazi waziri anayehusika na maendeleo ya uchumi na jamii kufuatia maandamano yaliyochochewa na uamuzi wa serikali kusitisha ruzuku ya mafuta.

Rais wa Angola, João Lourenço.
Rais wa Angola, João Lourenço. LUSA - AMPE ROGÉRIO
Matangazo ya kibiashara

Alimbadilisha Manuel Nunes Júnior, waziri mwenye uzoefu na profesa wa uchumi, na gavana wa benki kuu, José de Lima Massano, taarifa ilisema.

Uondoaji wa ruzuku,  ambao  Nunes Júnior alisema ulilenga kupunguza matumizi ya serikali,  ulianza kutekelezwa tarehe 1 Juni, na kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta.

Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu wakati huo limekuwa na wimbi la maandamano, huku zaidi yakitarajiwa mwishoni mwa juma.

Angola iliondoa ruzuku ya mafuta
Angola iliondoa ruzuku ya mafuta LUSA - AMPE ROGÉRIO

Siku ya Jumatatu, watu watano walifariki na wanane kujeruhiwa baada ya polisi kuwafyatulia risasi kundi la waandamanaji katika mji wa Huambo.

Angola ni mojawapo ya wauzaji wakubwa wa mafuta Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.