Pata taarifa kuu

Nambia kuwauza mamba 40

NAIROBI – Namibia imetangaza kwamba inawauza mamba 40 kama njia moja ya kupunguza mzozo kati ya binadamu na wanyama wa pori kaskazini mashariki mwa maeneo ya  Kavango na Zambezi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Wale ambao wanataka kuwanunua mamba hao wanatakiwa kuwa vyeti vya kuthibitisha kuwa watawalinda wanayama hao
Wale ambao wanataka kuwanunua mamba hao wanatakiwa kuwa vyeti vya kuthibitisha kuwa watawalinda wanayama hao Leigh Bedford / Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Wale walio na nia ya kuwanunua mamba hao, wanatarajiwa kuwasilisha maombi yao kwa wizara ya mazingira tarehe 17 ya mwezi Julai.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo Romeo Muyunda , sehemu kubwa ya wanayama pori nchii humo wanaishi nje wa mbuga za wanayama za kitaifa hali ambayo imepelekea ongezeko la wanayama hao kuwashambulia mifugo na binadamu  katika maeneo hayo.

Kabla ya kuwanunua wanayama hao, raia wametakiwa kuthibitisha kuwa wanasehemu maalum ya kuwahifadhi na watalipia gharama ya kuwakamata mamba hao.

Kwa wale ambao wanaolenga kuwanunua mamba hao wakiwa nje ya nchi, watatakiwa kuonyesha cheti kutoka kwa idara husika katika mataifa yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.