Pata taarifa kuu

Senegal: Macky Sall akabiliwa na mashitaka ya 'uhalifu dhidi ya binadamu'

Ombi la uchunguzi wa "uhalifu dhidi ya binadamu" limewasilishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya maafisa wa Senegal. Miongoni mwao ni hasa rais Macky Sall au Waziri wake wa Mambo ya Ndani na kamanda mmoja wa wa kikosi cha askari.

Rais wa Senegal Macky Sall, Februari 18, 2022.
Rais wa Senegal Macky Sall, Februari 18, 2022. AP - Johanna Geron
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Charlotte Idrac

Ni faili "ya kurasa 170" ambayo ilitumwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, kulingana na Juan Branco, wakili Mfaransa wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko. Anadai kupokea zaidi ya vielelezo 4,500 vya ushahidi kuhusu "uhalifu" uliofanywa nchini Senegal tangu mwezi Machi 2021.

Anataja makumi ya majina, ndani ya familia ya mkuu wa nchi, serikali, au hata vyombo vya usalama. "Tumefanya uchunguzi mrefu katika miezi ya hivi karibuni kwa kushirikisha mamia ya Wasenegal ambao umetuwezesha kubaini kuwepo kwa makosa 60 ya uhalifu, unaochukuliwa kuwa ni uhalifu dhidi yaubinadamu. Uhalifu huu ulifanywa kama sehemu ya shambulio la jumla na la kimfumo dhidi ya raia," wakili huyo ameelezea wanahabari.

Tunaomba uchunguzi wa awali na uchunguzi uanzishwe bila kuchelewa

Kwa hivyo utaratibu huo unahusu kipindi kati ya ghasia za mwezi Machi 2021 na ghasia za mwezi huu wa Juni, ambazo ziliua rasmi angalau watu 16, 30 kulingana na upinzani. Juan Branco sasa anaomba ofisi ya mwendesha mashtaka wa ICC kuchukua vielelezo hivi. Itakuwa juu ya Mahakama kuamua kufungua au kutofungua uchunguzi.

Madai hayo yalifutiliwa mabali na Waziri wa Majeshi na spika wa zamani wa Bunge la Nchi Wanachama wa ICC. Maitre Sidiki Kaba, wakati wa mkutano wa serikali na waandishi wa habari wiki jana alisema: “Tumesikia kwamba taifa la Senegal, mamlaka yake ya juu zaidi, itafikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Hizi ni ndoto. Wanaosema hivyo hawana ubora wala uwezo wa kufanya hivyo. Kuna mkanganyiko kwa sababu tunataka kuchafua sifa ya Senegal na kudhoofisha ari ya vikosi vya ulinzi na usalama”.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal, Aïssata Tall Sall, ameijibu RFI na France 24 kwa kuelezea madai haya kama "kejeli".

Kulingana na Juan Branco, malalamiko pia yamewasilishwa nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.